Wataalam wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka nchini Korea ya Kusini wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (NBS) yenye lengo la kujenga uwezo watumishi hao katika kuchakata taarifa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.

Akieleza kuhusu mafunzo hayo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka NBS Bw. Daniel Masolwa amesema kuwa mafunzo hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya nchini Korea ya Kusini.

" Mafunzo haya yatawezesha watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuongeza weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ", alisisitiza Masolwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Takwimu nchini Korea ya Kusini Bw. Charlse Seo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri katika ukusanyaji na uchakataji wa taarifa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.

"Ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Korea ya Kusini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) umejikita katika mafunzo ya kujenga uwezo na kutoa vifaa kwa NBS, aidha, mafunzo haya ni natokeo ya ushirikiano mzuri kati yetu", Alisisitiza Bw. Seo

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa ushirikiano kati ya NBS na Ofisi ya Takwimu ya nchini Korea ya Kusini Bw. Deogratius Malamsha amesema mradi huo ni wa miaka mitatu na ulianza mwaka 2021 na utakamilika 2023.

Watumishi 15 wa NBS wanashiriki mafunzo hayo ya wiki mbili yanayofanyika Dodoma.

Aidha, mradi huo unahusisha mafunzo na utoaji wa vifaa ambapo sehemu ya mafunzo yanafanyika Tanzania na mengine Korea ya Kusini.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ushirikiano kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Serikali ya Korea kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Korea Kusini.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...