Mwandishi wetu, Singida

KITUO cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) kimeanza kutoa bure ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili Hamis Mayombo amesema zoezi hilo ambalo limeanza jumatatu wiki hii litakuwa la wiki moja.

Wakili Mayombo amesema hadi Sasa mashauri mengi ambayo wamekuwa wakipokea ni migogoro ya ardhu,masuala ya mirathi na utawala bora, baadhi yatafikishwa mahakamani na mengine kupatiwa suluhu.

Wakili Mayombo ambaye ni Mkuu wa LHRC Ofisi ya Arusha, amesema mashauri ya ndoa yanatokana na migogoro ya kifamilia huku migogoro ya ardhi ikitokana na uvamizi wa ardhi.

Wakili Fides Mwenda amesema baadhi ya mashauri ambayo wamepokea tayari yamefikishwa mahakamani na mengine bado.

"lakini pia kuna malalamiko ya viongozi kukiuka misingi ya utawala bora hivyo wamelalamikiwa," amesema Mwenda.

Mmoja wa Wananchi hao, Michael Itembe amesema anataka msaada wa kisheria kusaidiwa kupata shamba lake ambalo limevamiwa na ndugu zake na kulima bila idhini yake.

"naomba LHRC isaidie kisitishwa kilimwa katika ardhi yangu hadi kesi ya msingi imalizike" amesema Itembe.

LHRC itatoa huduma za kisheria kwa wiki moja mkoani Singida.

Jumanne Issa ameeleza kuvamiwa ardhi yake na tayari shauri limefishwa mahakama I lakini hata hivyo bado suluhu haijapatikana.

Rehema Peter mkazi wilaya ya Ikungi ameeleza kusumbuliwa na ndugu wa marehemu mume wake katika suala la mirathi kwani wanataka kumnyang'anya mali zake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...