Na Jane Edward, Arusha


Chama Cha madaktari Tanzania kimetakiwa kuendelea kuhamasisha utoaji wa huduma ya chanjo ya uviko 19 kwenye vituo vya afya ili wananchi wote waone umuhimu wa chanjo hiyo.

Hayo yamesemwa na Daktari Omary Chande wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 54 wa kitaaluma wa chama Cha madaktari Tanzania unaofanyika jijini Arusha.
Chande amesema kwa Sasa unahitajika msukumo mkubwa kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupata chanjo ili huduma ya utoaji chanjo ya uviko iwe katika ubora unaotakiwa.

Aidha amewasihi madaktari kuendelea na kazi yao nzuri ya utoaji huduma Bora na kuheshimu taaluma na haki ya mgonjwa kupata matibabu inavyostahili kwa mujibu wa miongozo ya kitabibu.

Kwa upande wake Rais wa chama Cha madaktari Tanzania dokta Shedrak Mwaibambe amesema wamekutana kuangalia umuhimu wa utoaji wa chanjo ya uviko 19 awamu ya pili ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana kuhusu maadili wakati wa utoaji huduma kwa wagonjwa.

Amesema wamekuwa wakipokea malalamiko ya wagonjwa wakilalamikia utoaji huduma mbovu kutoka kwa watoa huduma za afya na kwamba kikao hicho miongoni mwa mambo watakayojadili ni kukumbushana maadili wanayotakiwa kutoa wakiwa na wagonjwa katika maeneo yao ya kazi.

Hata hivyo Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu Ni kuwa mapokeo ya chanjo ya uviko 19 na utayari wa kukubali kuchanja.

Rais wa chama cha madaktari Tanzania Shedrak Mwaibambe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Washiriki wakiwa  kwenye Mkutano Mkuu wa 54 wa chama cha madaktari Tanzania.

Mgeni rasmi wa Mkutano wa Chama cha madaktari Dr Omar Chande akikabidhi tuzo ya heshima kwa muwakilishi wa taasisi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza Bi Happy Nchimbi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...