*Waziri Mkuu afurahishwa na mchango wa JTI Leaf
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ameipongeza Kampuni ya JTI Leaf Services kwa mchango wake katika ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana katika kata ya Urambo, Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.
Mh. Majaliwa ametoa pongezi hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shula ya Sekondari ya Margaret Sitta huku akiongozana na Balozi wa Japan nchini Mh. Yasushi Misawa.
Alimpongeza Balozi huyo kwa mchango wa nchi yake kwa Tanzania. “Nchi yake imeendelea kudumisha mahusiano mazuri kwa kuleta makampuni kama JTI Leaf ambayo mbali na kununua tumbaku kwa wingi, wamekuwa wakishiriki katika miradi ya maendeleo,” alisema.
Alisema ujenzi wa shule hiyo ya wasichana ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Urambo lakini pia kwa watanzania kwa ujumla. “Hii ni zawadi kubwa kwa wananchi wetu na ni heshima kubwa kwangu kuja kuweka jiwe la msingi pamoja na Balozi,’alisema.
Kwa upande wake, Balozi Misawa alisema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii.
“Naiopongeza JTI Leaf kwa kuendelea kuwekeza katika jamiina naahidi kuwa serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na serkali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo,” alisema Balozi.
Naye Mbunge wa Urambo Mh. Margaret Sitta alisema shule hiyo ambayo ujenzi wake bado unaendelea, itasaidia kuwanusuru wanafunzi wa kike ambao wamekuwa wakikatiza masomo kwa sababu ya ujauzito.
Aliishukuru Kampuni ya JTI Leaf kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha shule hiyo inajengwa na pia aliipongeza serikali kwa kutoa eneo na watalaamu wa mradi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...