Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewahakikisha ushirikiano wa hali ya juu mabalozi ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Zimbambwe, Zambia pamoja na Uholanzi.

Ameyasema hayo katika mazungumzo yaliyofanyika Afisini kwake Vuga Jijini Zanzibar wakati alipokutana na mabalozi hao waliofika kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga baada ya kushika Wadhifa huo.

Mhe. Hemed amewataka mabalozi hao kwenda kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi ambazo wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwa kutumia mfumo wa kisasa kwa maslahi ya watanzania kwa ujumla.

Aidha amewataka mabalozi hao kwenda kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo katika nchi wanazokwenda kuitumikia Tanzania ili kuweza kuzifanyia kazi kwa lengo la kupata maendeleo endelevu.

Makamu wa Pili wa Rais amewataka mabalozi hao kuzitumia fursa za uwekezaji zilizopo Nchini na kuwakaribisha Wawekezaji kuja kuwekeza ili kukuza Uchumi wa Nchi pamoja kuitangaza Zaidi Tanzania.

Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kuwaasa mabalozi hao kuitangaza Tanzania kwa mazuri yake hasa Suala la Utalii na vivutio mbali mbali vilivyopo Nchini ili kukuza Sekta ya Utalii pamoja na kukuza pato la taifa.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka mabalozi hao kuamini kuwa watanzania wote wanawategemea kupitia nchi ambazo wanakwenda kuiwakilisha Tanzania ili wananchi kuweza kupata manufaa kupitia wao.

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake balozi ambae anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zambia Luteni General Mathew E.Mkingule amemuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa watahakikisha wanayatekeleza kwa vitendo yale yote ambayo wameagizwa na viongozi kwa maslahi ya watanzania wote.

Aidha Balozi Mkingule ameeleza kuwa watahakikisha lolote ambalo wanalifanya watafanya kwa maslahi ya watanzania huku wakiwa na kaulimbiu ya kuwa jamuhuri ya muungano kwanza.

Mabalozi waliokutana ni pamoja na malozi amaekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe IGP Mstaafu SIMON NYAKORO SIRRO

Balozi anaekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zambia Luteni general MATHEW E. MKINGULE, Balozi anaekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Uholanzi Bi CAROLINE KITANA CHIPETA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na mabalozi ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Zimbambwe, Zambia pamoja na Uholanzi waliofika kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga baada ya kushika Wadhifa huo Ofisini kwake Vuga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...