Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo (Tete a tete ) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres , Mazungumzo yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.
Hii leo tarehe 22 Septemba 2022 Makamu wa Rais akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaondelea nchini Marekani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres kabla ya mazungumzo yao yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro unaopatikana nchini Tanzania Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...