Njombe
Katibu
mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria nchini Bi.Merry Makondo amesema
serikali ya Tanzania inakwenda kufanya mapitio ya mfumo wa haki jinai
nchini ili kuhakikisha mashauri yote yanafanyiwa upelelezi kwa haraka
ili kuzisaidia Mahakama kuharakisha uendeshaji wa kesi na kutoa haki kwa
wakati.
Amebainisha haya
mkoani Njombe kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Dkt,Damas
Ndumbaro wakati wa maadhimisho ya miaka 27 ya kituo cha sheria na haki
za binadamu.
“Serikali
inaenda kufanya mapitio ya mfumo wa haki jinai nchini kuhakikisha kwamba
mashauri yote ya jinai katika ngazi ya uchunguzi,upelelezi,uendeshaji
wa mashtaka,utoaji wa ushahidi pamoja mashauri yanavyosikilizwa uweze
kuboreshwa na kuaptiwa ufumbuzi kwa haraka”amesema Bi.Makondo
Katika
kuhitimisha zoezi la utoaji wa msaada wa kisheria katika nyanja mbali
mbali kupitia kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) uliofanyika
mkoani Njombe wakati wa kuadhimisha miaka 27 ya kituo hicho,Mkurugenzi
wa kituo Bi.Anna Henga amesema wananchi 796 wamehudumiwa moja kwa moja
na mawakili wa kituo wakati wa maadhimisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...