Kutoka kushoto ni Mratibu wa chanjo Mkoa Dkt.Abbas Hincha katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt.Gunini Kamba na Mshauri GPEI,WHO ,IQVIA Dkt. Sally Emmanuel.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt.Gunini Kamba akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ofisi ya Mganga huyo zilizopo kwenye jengo la Mkuu wa Mkoa leo Septemba mosi, 2022.
Na Khadija Kalili, KIBAHA
MGANGA Mkuu wa mkoa wa Pwani Dkt. Gunini Kamba amesema kuwa hadi zoezi hili litakapokamilika wamejipanga kufikia lengo la kuchanja watoto kwa idadi ya 263,990.
Dkt. Kamba alisema hayo leo Septemmba Mosi, alipokua akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ofisi ya Mganga huyo zilizopo kwenye jengo la Mkuu wa Mkoa.
Dkt. Kamba alisema kuwa mwamko wa wazazi kupeleka na kujitokeza katika zoezi hili la chanjo ya Polia ni mkubwa na unaridhisha.
Aidha chanjo hii imeanza kutolewa rasmi kitaifa leo nchi mzima ambapo chanjo hii ni muhimu kwa watoto kwa sababu kama mlivyosikia hivi karibuni kumetokea mlipuko qa ugonjwa wa Polio uliotokea katika nchi jirani ya Malawi Februari mwaka huu" alisema Dkt. Gunini.
"Ni muhimu kila mtoto apate chanjo hii ili kuimarisha kinga yake na kuzuia ugonjwa usiingie nchini" alisema Dkt.Kamba.
Dkt. Kamba amesema kuwa chanjo hii ya ugonjwa wa Polio ni zawadi ya maisha kwa mtoto hivyo sote inatupasa tuelewe kuwa jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya bora kwa maendeleo ya Taifa.
Alisemakuwa anatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa timu za wachanjaji watakapofika katika maeneo yao na kupita kwenye nyumba ili kutoa matone ya chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya miaka mitano kutoa ushirikiano.
Amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka mwaka huu "Kila tone la chanjo ya Polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza" alisema Dkt.Gunini
Amesema kuwa tayari wamefanya vizuri katika awamu ya pili kwa kuvuka lengo la uchanjaji kwa asilimia131 ya walengwa wote na hivyo tunatarajia kufanya vizuri zaidi katika awamu hii ya tatu huku akifafanua kwa kuwatoa hofu wazazi na wananchi kwa ujumla kuwa chanjo hii ya Polio haina madhara yoyote
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...