Njombe
Mkuu
wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa wito kwa watu wanaoishi na
maambukizi ya virusi vya ukimwi kuacha kuogopa kutumia dawa za kufubaza
maambukizi kwa kuwa serikali imetatua changamoto ya kukosekana kwa dawa
hizo huku akiwataka kuacha kuchanganya ARV's na dawa za kienyeji.
Aidha
mkuu huyo wa wilaya mara baada ya kukagua shughuli za maendeleo
zinazofanywa na vikundi vya WAVIU kupitia konga za halmashauri ya wilaya
ya Njombe,amesema ni hatari kwa watu kunywa dawa kwa kificho kwa kuwa
wamekuwa wakijisababishia matatizo makubwa.
“Ukiacha
dawa ghafla kuna madhara makubwa na wengine wanachanganya na dawa za
kienyeji,lakini kuna hawa wanaokunywa dawa kwa kificho hii ni hatari
zaidi kwasababu unapoenda kliniki unapimwa na wataalamu wanajua kama
kuna haja ya kukubadirishia dawa,wengine wamefikia hatua ya kununua
wenyewe dawa za nje zisizokuwa na kipimo na kupata madhara”amesema Kissa
Kasongwa
Mganga mkuu wa
halmashauri ya wilaya ya Njombe Dkt,Suke Magembe ametoa ushauri kutumiwa
dawa zilizothibitishwa na mkemia mkuu ili kuepukana na madhara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...