Mufti wa Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) akiongoza kuomba dua baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa katika hafla iliyofanyika leo Septemba 18, 2022. Kutoka kulia Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau, Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.


Mufti wa Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (kushoto) akiwa na viongoziwengine katika hafla hiyo. Kutoka kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

Mufti wa Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akizungumza na Waislam wakati alipotembelea Taasisi wa Majmaul Ahbaab..

Mufti wa Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akionesha Tuzo ya heshima baada ya kutunukiwa na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh (kushoto).



Vijana wa Skauti wakiwa katika ziara hiyo ya Mufti.

Wanawake wa kiislam wakimsikiliza Mufti wa Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir wakati alipotembelea Taasisi ya Majmaul Ahbaab.

Hafla ikiendelea.

Vijana wa Qaswida wakiwa nadhifu wakati wa hafla hiyo .
...............................................





Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida

MUFTI wa Tanzania sheikh Dk.Abubakar Zubeir leo Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa.

Azungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema amefurahishwa na ridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotakiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

"Mimi na msafara wangu masheikh wote waliofika katika kutekeleza mambo yetu hapa Singida tumefurahishwa sana na jambo hili na haya ndio mambo yetu ya bakwata tunayoyazungumza sana kuhusu maendeleo" alisema Mufti Zuberi.

Mufti Zuberi alisema changamoto zote zilizotolewa katika hafla hiyo alisema baraza na viongozi wapo hivyo wanaona namna ya kuzishughulikia na kuwekana sawa kwani kila jambo lina taratibu zake namna ya kuzitatua.

Aidha Mufti Zuberi alisema jambolililokubwa ni kwa waislam mkoani hapa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awawezeshekufanya mambo yao vizuri na kuondosha magomvi baina yao.

Taarifa ya ujenzi huo ikitolewa mbele ya Mufti ilieleza kuwa Mwezi Marchi 2022 Sheikh wa Mkoa wa Singida na Baraza la Masheikh waliunda kamati maalumu ili kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa eneo la ujenzi na kufanikiwa kuipata ndani ya Masjid Taqwa kwa idhini ya uongozi wa msikiti huo.

Ujenzi wa ofisi hiyo hivi sasa umefikia hatua ya linta kwa gharama ya Sh.8.2 mILIONI na kaziiliyobakia ni upauaji na umaliziaji ambapo fedha zilizokadiriwa kumalizia kazi hiyo ni Sh.14 Milioni.

Mufti akiwa njiani kwenda Singida mjini alisimama wilayani Ikungi na kuomba dua kwenye eneo ambalo waislam wa wilaya hiyo wanatarajia kujenga Kituo cha afya na baada ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi la ofisi ya Bakwata alikwenda kutembelea Taasisi ya Majmaul Ahbaab iliyopo eneo la Unyakhindi Manispaaya Singida ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanawake wa kiislam na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa na Rais wa Taasisi hiyo Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...