Na Mwandishi Wetu Dodoma


Wakati Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikichanganua fedha za Uviko-19, Sh203.14 bilioni zilivyotumika, Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi vifaa tiba vilivyonunuliwa kutokana na sehemu ya fedha hizo.

Hayo yamefanyika leo Ijumaa Septemba 30, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe.

Akitoa maelezo, Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, Dk Grace Maghembe amesema walipokea Sh203.14 bilioni ambapo sehemu ya fedha hizo zilitumika katika ujenzi wa majengo ya dharura yaliyojengwa katika halmashauri 80 nchini.

Amesema vigezo vilivyoangaliwa katika kuchagua maeneo ya kujenga ni wingi wa magonjwa ya dharura, umbali wa upatikanaji wa huduma.

Amesema vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) 26 vimejengwa, kutengeneza mitambo ya kuzalishia gesi 20, vifaa vya upasuaji taa na vitanda na vifaa vyake, vifaa tiba mchanganyiko vyote 184.

Dk Grace amesema pia wamenunua machine za mionzi (X-Ray) 137 ambazo zitakwenda katika hospitali zote za wilaya zilizokuwa hazina mashine hizo.

Amesema mashine za mionzi zitakazobakia zitakwenda kuwekwa katika vituo vyote vyenye wagonjwa wengi vikiwemo barabarani ambapo watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha.

Awali Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amesema hafla ya kutiliana saini kwa Serikali na wakuu wa mikoa kwa lengo la kuimarisha masuala ya kupunguza matatizo ya lishe ni ya sita tangu utaratibu huyo uanze.

Amesema katika hafla hiyo, pia Rais Samia Suluhu Hassan atazindua magari 52 kati ya 200 kwa ajili ya maofisa elimu sekondari.

Pia atagawa pikipiki 517 kwa ajili ya kufuatilia lishe na vifaa tiba kwa ajili ya zahanati na vituo vya Serikali za mitaa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema changamoto iliyopo nchini sasa ni watu kutokuwa na uelewa wa lishe.

“Dodoma mwaka 2018 wakati tathimini inafanyika ilikuwa chini lakini naamini kuwa tathimini ikifanyika sasa hivi itakuwa imepanda,”amesema Senyamule.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe ya vifaa tiba Vipya ambavyo ni meza za upasuaji 79, taa za upasuaji 79, mashine za kutoa dawa za usingizi 10, mashine 82 za kidijitali za X-ray na seti ya samani 1,006 ya vitanda vya wagonjwa, magodoro na makabati ya vitanda vitakavyosambazwa kwenye vituo vya huduma za afya nchi.

Rais amepokea malezo hayo wakati akikagua mabanda katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Usimamizi wa shughuli za Lishe na tathmini ya Sita (6) ya Mkataba wa Lishe uliofanyika Ukumbi wa Jiji la Dodoma - Mtumba. Leo tarehe 30 Septemba 2022 (Picha na Eliud Rwechungura - OR TAMISEMI)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...