RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya msiba wa Malkia Elizabeth II.


Siku ya Jumapili, viongozi mbalimbali walioalikwa akiwemo Rais Samia watatoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia atatia saini kitabu cha maombolezo.


Baada ya hatua hiyo Rais Samia atahudhuria hafla fupi ilioandaliwa na aliyetamkwa kuwa Mfalme Charles III ambaye amemrithi mama yake Marehemu Malkia Elizabeth II.


Hafla hiyo ambayo pia imeandaliwa na Malkia Mfariji (Queen Consort), Camilla Parker Bowles itafanyika katika Kasri ya Buckingham jijini London.

Aidha, siku ya Jumatatu, Rais Samia atahudhuria Mazishi ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth II yatakayofanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey. Mwili wa Malkia Elizabeth utalazwa kwenye kasri la Windsor.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...