Njombe


Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema hapendi kuona mabango yanayotangaza kuongeza nguvu za kiume au kusafisha nyota sambamba na matangazo mengine yanayofanana na hayo katika maeneo ya mkoa huo badala yake anataka kuona mabango yanayohusu elimu ili kuongeza taaluma kwa wanafunzi.

Mtaka amebainisha hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wa mkoa huo katika hafla ya uzinduzi wa kifurushi maalumu kilichotolewa na benki ya NMB kwaajili ya kuwasaidia walimu kuepukana na mikopo umiza.

“Unaenda kwenye mitaa unakuta bango tunasifisha nyota,hivi tuko siliasi! Hapana tusiende huko mimi nataka nikipita barabarani nione bango kubwa Pre-Form One, haya ndio ninayoyataka kuona”amesema Mtaka




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...