Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA ), Bi. Angela Anatory amewataka wananchi kuendelea kufika katika ofisi za RITA zinazopatikana katika maeneo yote Tanzania Bara ili kuweza kukamilisha mahitaji yao ya msingi katika jamii.
Bi. Angela amesema hayo kwenye mkutano mkuu wa mawakili wa Serikali ya Tanzania uliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 hadi 30 Septemba 2022 katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Centre jijini Dodoma.
"Kama inavyojulikana ya kuwa ofisi za RITA zipo katika kila jengo la mkuu wa wilaya Tanzania Bara pamoja makao yake makuu Dodoma na Dar es Salaam hivyo basi kupitia mkutano huu wa mawakili wa serikali ya Tanzania ambapo pia wakala tunatoa huduma ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa na huduma zetu nyingine nawasihi wananchi waendelee kufika RITA na kujipatia huduma zetu ili waweze kukamilisha mahitaji yao muhimu kama vile elimu, ajira, kupata matibabu kwa kupitia cheti cha kuzaliwa" alisema.
Akiwa katika banda la RITA Bi. Angela ameshiriki kutoa huduma na kusikiliza maoni ya wananchi wakati wakipatiwa huduma bandani humo kama sehemu ya kutathimini hali ya utoaji wa huduma mbalimbali za Wakala ili kuboresha maeneo yatakayoonekana kuwa na changamoto ya kukwamisha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
"Nawaomba sana Wananchi, sisi tupo tayari kuwahudumia na ofisi zetu zipo wazi masaa ya kazi lakini pia unaweza kupata huduma zetu kwa njia ya Kielektroniki kupitia E-Huduma na ukapata cheti cha Kuzaliwa au kifo na hata kusajili Bodi za Wadhamini kwa njia ya mtandao". Alisema Bi. Anatory.
Aidha, mbali na kutoa huduma ya usajili wa cheti cha kuzaliwa Wakala umetoa huduma ya msaada wa kisheria kuhusu masuala ya Wosia na Mirathi lakini pia elimu kwa umma kuhusu usajili wa Ndoa,Talaka,Ufilisi na Udhamini. Mgeni rasmi katika mkutano huo wa mawakili wa serikali ya Tanzania alikuwa ni Mheshimiwa Rais Samia Suluhu.
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Bi. Angela Anatory akihudumia wananchi katika banda la RITA kwenye mkutano mkuu wa mawakili wa serikali ya Tanzania uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Conventional Centre, Dodoma.
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Bi. Angela Anatory akihudumia wananchi katika banda la RITA kwenye mkutano mkuu wa mawakili wa serikali ya Tanzania uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Conventional Centre, Dodoma.
Baadhi ya mawakili wa serikali kutoka ofisi ya RITA wakiwa katika ukumbi wa mkutano mkuu wa mawakili wa serikali ya Tanzania.
Wananchi wakipata huduma katika banda la RITA
Wananchi wakipata huduma katika banda la RITA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...