Na. OMM Rukwa

Afisa Mpango wa Taifa wa Afya Shuleni toka Wizara ya Afya Dkt. Emmanuel Mnkeni amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kudhibiti mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu.

Dkt. Mnkeni alisema mafunzo kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ( CHWs), Walimu na Wenyeviti wa kamati za Shule yanalenga kuhamasisha jamii kuhusu ujenzi wa vyoo bora na usafi wa mazingira ili kudhubiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Mafunzo hayo yametolewa Leo ( 27.09.2022) katika kijiji cha Kirando Wilaya ya Nkasi ambapo Wizara ya Afya inalenga kuhamasisha na kuelimisha viongozi na jamii kushirikiana ili kuweka utamaduni wa kutumia vyoo bora.

" Wizara ya Afya kwa kushirikana na OR- TAMISEMI inaendelea kutoa elimu endelevu ili jamii iweze kubadilika kwa kutumia vyoo bora,kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kunywa maji safi na salama" alisema Dkt. Mnkeni.

Kwa upande wake Peter Muna ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Mkinga alisema Sheria ndogo ziendelee kutumika hata pale ugonjwa wa kipindupindu unapoisha na kuwa viongozi wa vijiji wawe mfano wa kuigwa kwa kuwa na vyoo safi na kuvitumia.

Naye Mwalimu Betty Sungura toka Shule ya Msingi Mpata kata ya Kirando aliiomba serikali iongeze nguvu katika upatikanaji wa miundombinu ya kutosha ya matundu ya vyoo ili watoto waepuke mlundikano wanapoenda chooni.

" Miundombinu mibovu ya vyoo kinakuwa chanjo cha mlipuko wa magonjwa hususan pale shule inapokuwa na msongamano wa watoto" alisema Mwalimu Sungura.

Kwa upande wake Afisa Elimu ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Augustine Bayo alibainisha kuwa viongozi wa vijiji na kata ndio wenye jukumu la kuhakikisha wanafunzi wakuwa na vyoo bora na vinatumika .

Bayo aliongeza kusema serikali inajitahidi kutenga fedha za kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya vyoo kupitia mradi wa SWASH.

"Kila kaya au shule lazima iwe na vyoo bora ili kudhibiti mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu " alisema Bayo.

Wilaya za Nkasi na Kalambo kwa nyakati tofauti zimekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bakteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam " Vibrio cholera" na madhara yake ni pamoja na vifo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...