Na. Jeremiah Mbwambo, BMH- Dodoma
Wazazi wamejitokeza kwa wingi kupeleka watoto kuchunguzwa na kutibiwa magonjwa ya Moyo kwenye kambi ya uchunguzi na matibabu ya Moyo inayoendelea katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Moyo wa Hospitali hiyo wameungana na wenzao kutoka Shirika lisilo la kiserikali la One New Heart Foundation pamoja na wengine kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando kufanya uchunguzi na kutibu watoto wenye matatizo ya Moyo kwa siku 5.
Jumla ya watoto 68 walifanyiwa uchunguzi wa matatizo mbalimbali ya Moyo tangu Septemba 26 hadi kufikia leo Septemba 29, asilimia 91 wamekutwa na matatizo ya Moyo ya kuzaliwa nayo ikiwemo Matundu kwenye Moyo, Matatizo kwenye mishipa ya Moyo na Matatizo kwenye njia ya Moyo.
Hii ni mara ya nne tangu kuanzishwa ushirikiano wa kutoa huduma za Moyo kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Shirika lisilo la kiserikali la One New Heart Foundation.
Kati ya hao 25, watoto 18 walifanyiwa matibabu ya upasuaji kwa njia ya Matundu kupitia mshipa wa paja kwa kutumia Maabara maalumu ya Uchunguzi na Matibabu ya Moyo (Cath-Lab) iliyopo Hospitalini hapo, ambapo watoto 7 walifanyiwa matibabu ya upasuaji wa kufungua kifua. Dunia inapoadhimisha siku ya Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma Dkt. Alphonce Chandika, anatoa wito kwa watanzania kujikinga dhidi ya maradhi ya Moyo kwa Kufanya Mazoezi, kupunguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi, kucha matumizi ya sigara, kupunguza matumizi ya Pombe, kuchunguza Afya zao mara kwa mara na kwa wagonjwa kufuata maelekezo ya wataalamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...