Na Mwandishi wetu
KATIKA kuhakikisha vipaji vinaendelea kukuzwa nchini, Taasisi ya Hakika Tunajifunza kwa kushirikiana na Kampuni ya Ushauri wa Kitaalamu ya GJS wameandaa kampeni maalum ya kutoa elimu ya mazingira na afya kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini.

Kampeni hiyo itakayokwenda sambamba na ufanyaji wa mazoezi ya viungo inatarajiwa kufanyika Septemba 10, mwaka huu katika shule ya Sekondari Makurumla iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampeni ya Hakika Tunajifunza, Furaha Mbakile amesema kampeni hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wafanyao mazoezi ya kujenga mwili pamoja na kupata elimu hiyo ya mazingira na afya.

Amesema kampeni hiyo itafanyika katika shule mbalimbali zilizopo kwenye wilaya tano za jijini Dar es Salam ambapo mbali na mazoezi watapata fursa ya kushiriki kongamano litakaloongozwa na Mwandishi Mkongwe Jenerali Ulimwengu.

"Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Julai 27, 2022 ina lengo la kwenda sambamba na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anakauli mbiu yake ya kutaka kazi kuendelea hivyo na sisi tunataka wanafunzi waendelee kujifunza.

"Hapa Dar es Salaam tutakwenda shule zote zilizopo kwenye wilaya tano na tutafanya kongamano maalum ambao Jenerali Ulimwengu atakuwepo kuzungumza masuala ya mazingira na umuhimu wa kutunza afya," anasema

Naye Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Ushauri wa Kitaalamu ya GJS, Mchungaji Mstaafu Joseph Chaggama alisema watashirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Serikali katika kufanikisha kampeni hiyo.

Alisema vipo vitu vingi vya kujifunza katika soko uliya mahali ambapo wema unaweza kuuzwa hivyo wananchi hasa wanafunzi ni muhimu wakapata elimu hiyo ya mazingira na afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...