KAULI MBIU: 'Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu'

Taasisi za Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) na Plan International Tanzania zimeandaa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kujiamini kwa watoto wa kike 40 juu ya kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi juu ya maswala hayo.

Mafunzo hayo, ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani, yatafanyika mnamo Septemba 24, 2022 katika hoteli ya Regency jijini Dar es salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni imelenga ile ile ya kimataifa ya: “Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu”

“Mafunzo hayo yataenda kwa jina la “Wasichana Washika Hatamu” na ni jukwaa la kuwapa mafunzo Watoto wa kike ya kuongeza uwezo wa kujiamini ,kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi katika nafasi za kufanya maamuzi”, anasema Mtendaji Mkuu wa JMKF, Bi. Vanessa Anyoti.

Bi Anyoti amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike imekuwa jukwaa muhimu katika kutambua haki za msichana pamoja na changamoto kubwa anazopambana nazo duniani, na kwamba sasa kuna wito wa kuchukuliwa kwa hatua za makusudi za kuleta mageuzi kijamii na kisiasa ili kuondoa vizuizi mbalimbali vya ubaguzi na chuki vinavyoendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wasichana.

“Tanzania inaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala yanayowakabili wasichana na kuwapatia fursa ya kupaza sauti zao.

“Duniani, wasichana wanaendelea kukabiliana na changamoto za uongozi, elimu, masuala ya afya ya akili na ukatili wa kijinsia, wakati wao ndio mawakala wakuu wa mabadiliko katika jamii zao”, anaongezea Bi. Anyoti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...