Na Janeth Raphael - Michuzi TV DODOMA
TAASISI ya kuzuia na Kuapambana na rushwa nchini TAKUKURU imeshauriwa kuwa na vikao kazi na semina ili kuwajengea uelewa watumishi wa Umma hasa katika maeneo ya manunuzi ili miradi inayofanyika iendane na thamani halisi ya fedha ili kuondokana na rushwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri alipotembelea Mabanda mbalimbali kwenye wiki ya maonesho ya maadhimisho ya Miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utaswala bora yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete ambapo Taasisi mbalimbali za Msaada wa sheria zimeshiriki.
“Lazima tukiri kwamba kuna changamoto kwenye sehemu ya rushwa , vitu viwili naendelea kusisitiza cha kwanza kumlea samaki akiwa mchanga, wanafanya kazi nzuri na mimi kwenye wilaya nimeandaa midahalo tunashindanisha shule kwenye kupinga masuala ya rushwa kwa njia ya mdahalo,
Tunawakutanisha wanafunzi wanafanya midahalo tunawajenga wakiwa wadogo ili wanapokuwa wajie nchi yao inatakiwa kuwaje”anasema Shekimweri
Aidha Shekimweri amewataka wananchi kujitokeza kwenda kupata elimu juu ya haki mbalimbali ambazo zinatolewa katika viwanjka vya Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Bunadamu na Utawala bora,Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa kama Tume wamekuwa wakipokea malalamiko mbalimbali yakkiwemo ya migogoro ya ardhi,Jeshi la polisi kulalamikiwa kubambnikiza kesi pamoja na kutesa wananchi ikiwemo na masuala ya rushwa.
“Nyakati hizi naona malalamiko ya migogoro ya ardhi yanayoletwa si mengi sana lakini yale machache yanayotufikia tumeyashughulikia kwa kufanya chunguzi na kutoa mapendekezo kwa taasisis husika nakuyachukulia hatua,
Kuhusu masuala ya unyanyasaji haya mara nyingi yakija kwetu kule polisi kuna dawati,tunayapeleka dawati la jinsia na wao wenzetu wanaanzisha mchakato wa upepelezi” amesema Jaji Mwaimu
Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kaulimbiu isemayo” Miaka 20 ya kuhamasisha ulinzi wa hifadhi ya Haki za binadamu na misingi ya utaswala bora.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akizungumza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya wafanyabiadhara kuelekea wiki ya maadhimisho ya miaka 20 ya Tume za haki za binadamu na utawala bora jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akizungumza na wanahabari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...