
Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Kimataifa-TALGWU Shani Kibwasali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 huku Chama kikiwa na mafanikio ya kiutendaji katika kuangalia maslahi ya wafanyakazi.
*Wadai wanafatilia masuala hayo serikalini kwa kutoa ushauri maboresho ya sheria ya tozo kwenye benki.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimesema kuwa wafayakazi watulie kuhusiana na tozo za miamala ya benki kwani wamefikisha maombi serikalini kufanya mabadiliko ya sheria ya tozo ili kuepuka malipo ya mara mbili kwenye mshahara wa mtumishi wa umma.
Hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Kimataifa-TALGWU Shani Kibwasali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 huku Chama kikiwa na mafanikio ya kiutendaji katika kuangalia maslahi ya wafanyakazi.
Shani amesema tozo za mara mbili kwa mfanyakazi ni mzigo kutokana na mishahara yao kuwa midogo ambao haukidhi mahitaji ya kila Siku na familia zao.
Amesema tozo za kibenki lililoanza kutekelezwa hivi karibuni zinawaathiri sana wanachama wetu kwa kila mwezi wanalipa Kodi kwa kukatwa katika mishahara yao.
“Lakini sasa kuanza kuanza kutekelezwa kwa tozo ya Serikali kwa miamala ya kutoa na kuhamisha fedha katika benki inamfanya mtumishi wa umma kutozwa zaidi ya mara mbili katika kipato moja kwa mwezi, ambacho hicho hicho kinachokatwa ni kidogo”.amesema Shani
Aidha amezungumzia suala la nyongeza ya mishahara a kubainisha kuwa wanachama wao ni wahanga wakubwa kwani bado kuna manung’uniko ya nyongeza hiyo ya mshahara.
"TALGWU kama msemaji wao hawajaridhika na nyongeza ya mshahara ilivyofanyika" amesema Shani.
“Naomba niwatoe hofu wanachama wetu kwamba suala hili linashughulikiwa na Chama kwa kushirikiana na shirikisho la vyama huru vya Wafanyakazi nchini (TUCTA),”.amesema Shani
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya TALGWU kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, amesema kwamba hadi kufikia Juni 2022 walikuwa na jumla ya kesi 140 ambapo mawakili wa Chama wanasimamia kesi 100, mawakili wa nje wanasimamia kesi 13, na rufaa zilizopo Tume ya Utumishi wa Umma ni 27.
Amesema Chama kiliandaa utetezi kwa watumishi 12 waliokuwa wamepewa mashataka na waajiri.
Shani amesema kati ya kesi 140 walizonazo zilizoisha zilikuwa ni 39 na chama kimeshinda jumla ya kesi 35 na kushindwa kesi nne huku kesi nyingine zikiendelea Mahakamani.
Amebainisha kuwa katika kipindi hicho pia TALGWU ilikuwa na jukumu jingine kubwa la kushughulikia haki na stahiki za wanachama ambazo kimsingi zipo kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake.
Hata huvyo amesema TALGWU inajivunia kuona Serikali imetekeleza maombi yao katika maeneo ya upandiahaji vyeo na mishahara, malipo ya malimbikizo ya mishahara na utawala Bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...