Na Khadija Seif, Michuzi Tv
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya utanashati, urembo na mtindo (Miss & Mister Deaf) kwa watu wenye matatizo ya kusikia ‘Viziwi’.

Mashindano hayo yanatarajia kufanyika Oktoba 23 hadi 31 mwaka huu katika Ukumbi wa Peacock Hoteli uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA), Habibu Mrope amesema mashindano hayo yatashirikisha washiriki 200 kutoka nchi mbalimbali.

“Mpaka sasa washiriki 160 wamejiandakisha kushiriki mashindano haya, hapa nchini tunawashiriki sita ambapo wavulana wawili na wasichana wanne".

Aidha ameeleza Tanzania kuchaguliwa kuandaa mashindano hayo kutokana na amani, vivutio vya utalii, ukarimu na ushirikiano mzuri uliopo nchini.

“Tulichaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano kutokana na ukarimu mzuri tuliokuwa nao, pia vivutio vya utalii wetu kama Mlima Kilimanjaro."

Mwenyekiti huyo amewataja Miss & Mister Deaf ambao wataiwakilisha Taifa katika mashindano hayo ni Khadija Kanyama, Joyce Denis, Carlyone Mwakasaka, Durath Mwankis, Rajabu Ali na Russo Songoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...