Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akimsikiliza daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela (kulia) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza kesho tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini humo ambao wako katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022.

Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akisalimiana na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo, madaktari wa watoto kutoka nchini humo na viongozi wa JKCI mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimwelezea Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa ziara yake aliyoifanya leo JKCI kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo ya matibabu itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Picha na Khamisi Mussa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...