Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika ambazo zinatekeleza dhana ya ushirikishwaji wa Jamii katika uhifadhi wa kivitendo kwa kutoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika kusimamia rasilimali za wanyamapori

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi wakati akifungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha

Amesisitiza kuwa WMAs ni kinga (buffer) muhimu kwa maeneo ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Ngorongoro na Mapori Tengefu.

Mkomi amesema bila WMAs changamoto za kiuhifadhi zitaathiri moja kwa moja Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Ngorongoro na Mapori Tengefu

Kutokana na umuhimu huo, Mkomi ametoa wito kwa Wadau wa Uhifadhi nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza WMAs ili kuziwezesha kujisimamia na kujiendesha.

Ameongeza kuwa kupitia ushirikishwaji huo Jamii zimekuwa zikinufaika na matunda yatokanayo na shughuli za uhifadhi katika maeneo yao kwa kujiletea maendeleo na huduma za kijamii ikiwemo shule na zahanati

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha amesema toka kuanzishwa kwa dhana ya WMAs jamii imekuwa ikishiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori hali inayopelekea ulinzi wa kuwa madhubuti

Amesema kufuatia hali hiyo maeneo ya WMAs yamekuwa ya kuvutia shughuli mbalimbali za uwekezaji kwa ajili ya utalii wa picha, uwindaji wa kitalii na uwekezaji kwa ajili ya hewa ya ukaa

Akizungumzia manufaa ya ushirikishwaji huo, Dkt. Msuha amesema katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2021 jumla ya jumuiya 15 zenya mikataba ya uwekezaji katika uwindaji wa kitalii zimeweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 4.91 ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ufadhili wa wanafunzi kusoma katika vyuo vikuu


Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akizungumza wakati akifungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha akizungumza kabla ya kumkaribisha aibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi kwa ajili kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori nchini John Salehe wakati wa hafla ya kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi UNDP, Gertrude Lyatuu akizungumza wakati wa hafla ya kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha ambapo amewataka Wadau hao kuwa mstari wa mbele katika kulinda maeneo ya Hifadhi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori nchini John Salehe akizungumza mbele ya Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi (kulia) ambapo ameushukuru Uongozi wa Wizara wa Maliasili na Utalii kwa kuendelea changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiikumba Jumuiya za Wanyamapori nchini
Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti wa Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) mara baada ya kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya maandalizi mara baada ya kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...