Kufuatia mwaliko wa Mwenyekiti wa Emirates Falconer’s Club Sheikh Hamdan Bin Zayed Al Nahyan, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki maonesho ya kimataifa ya uwindaji wa kitalii na waendesha farasi ( Abu Dhabi International Hunting and Equestrian Exhibition-ADIHEX-2022) yanayofanyika katika viwanja vya kimataifa vya maonesho Abu Dhabi nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE).

Maonesho hayo hufanyika kila mwaka na hukutanisha watu zaidi ya 105,000 kutoka nchi zaidi ya 120 kwa lengo la kukuza na kutangaza uwindaji endelevu wa wanyamapori duniani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na TAWA,imeeleza kuwa inatumia maonesho hayo kutangaza fursa za uwekezaji ikiwa ni pamoja na uwindaji wa kitalii katika maeneo inayo simamia.

Maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 26 Septemba 2022 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 02 Oktoba 2022.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...