Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV Kagera

Shirika la Viwango Nchini Tanzania limeendelea na Utoaji Elimu kwa Maafisa Upimaji wa Mkoa Kagera, juu ya mafunzo maalumu ya kuhusu Sayansi ya Vipimo.

Mafunzo hayo ya Siku Mbili yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila, katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba Septemba 09 Mwaka huu yakiwa na Lengo la kuwafundisha maafisa hao kutoka Taasisi na Mashirikia mbalimbali, namna ya kutambua usahihi wa Vifaa vinavyotumika katika Vipimo (ugezi) pamoja na Sayansi ya Vipimo (Metrolojia) yakiwa ni Mambo muhimu katika uzalishaji na Utoaji Huduma.

Mhe. Machali pamoja na Mambo mengine amewataka Washiriki wa semina hiyo Kuhakikisha wanaitendea haki kwa kuisambaza Elimu hiyo watakayoipata kwa jamii inayowazunguka badala ya kukumbatia kwa manufaa yao binafsi

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali akihutubia wakati wa UFUNGUZI wa Semina kwa Maafisa Upimaji Mkoa wa Kagera katika Ukumbi wa Bukoba Manispaa

Meneja wa Huduma za Metrolojia na Ugezi kutoka TBS,Bi Stella Mrosso akieleza lengo la Semina

Afisa Metrolojia kutoka TBS,Ndg. Joseph Kadenge akifundisha Mada ya Mifumo wa Metrolojia




Baadhi wa Washiriki wa Semina kutoka Taasisi na Mashirika mbalimbali wakiendelea na Mafunzo ya Metrolojia Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...