Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, amefungua kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar Es Salaam leo tarehe 23/09/2022.

Akifungua kikao hicho, Mrajis alieleza kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeandaa Taarifa ya Utendaji wa SACCOS kwa mwaka 2021 (The SACCOS Annual Performance Report 2021) yenye lengo la kupima utendaji wa shughuli za SACCOS kwa mwaka 2021. Taarifa hiyo itakuwa inaandaliwa kila mwaka.

Dkt. Ndiege amesema mkakati huu utasaidia SACCOS kuweka mipango yenye ufanisi yanayopimika katika utekelezaji wa shughuli za Chama ili kufikia malengo waliyojiwekea.

"SACCOS zinaendeshwa kwa kuzingatia Mifumo iliyowekwa na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na Miongozo mingine inayotolewa kwa Maendeleo ya SACCOS nchini, na hii inapelekea Vyama kuendelea kusajiliwa na kukua kwa kasi zaidi," amesema Dkt. Ndiege.

Alisisitiza kuwa ni jukumu la Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuendelea kusimamia na kuhamasisha Maendeleo ya Ushirika ili kuondoa taswira mbaya iliyojengeka kwa jamii kuwa Ushirika haufai kwa kuweka mifumo thabiti na kuonesha manufaa ya Vyama vya Ushirika kupitia mafanikio na masuala mazuri yanayofanyika ndani ya Sekta ya Ushirika.

"Ushirika husaidia wanachama kuinua uchumi wao na kujiendeleza kwa masuala ya Maendeleo kama vile kusomesha, kujenga na kuanzisha biashara," alisema Dkt. Ndiege.

Vilevile Mrajis alisema kuwa ni wakati wa SACCOS zote nchini kuanzisha Mfuko wa Kinga za Akiba na Amana. Mfuko huo utakuwa na faida kwa wanachama wote na endapo SACCOS ikishindwa kujiendesha Mfuko huo utasaidia kuwalipa wanachama fedha ambazo walizoweka kwenye SACCOS. Hivyo aliwataka washiriki kujadiliana na kutoa maoni juu ya uanzishwaji wa Mfuko huo.

Pia, amewataka Viongozi wa SACCOS kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali iliyotolewa na Mrajis ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Dkt. Ndiege aliwasisitiza Wanaushirika kuwa wakifanya kazi kwa kufuata miongozo na kwa uwazi Vyama vitafanikiwa katika nyanja zote na kujibu mahitaji ya wanachama wao.


Aidha, Mrajis amezitaka SACCOS zote na Wadau wa Maendeleo ya Ushirikia kuendelea *kununua Hisa katika Benki ya Ushirika ya KCBL itakayopelekea kuanzishwa kwa Benki ya Taifa ya Ushirika (NBCT)* ambayo itasaidia kuimarisha
Sekta ya Ushirika ikiwemo Ushirika wa SACCOS
 .

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, akifungua kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar Es Salaam leo tarehe 23/09/2022


Washiriki wa vyama vya Akiba na Mikopo wakiwa katika kikao kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar

Washiriki wa vyama vya Akiba na Mikopo wakiwa katika kikao kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar

Washiriki wa vyama vya Akiba na Mikopo wakiwa katika kikao kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar

Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga akiwasisitiza washiriki wa kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS huru na kutoa maoni na mawazo yenye tija ambayo yatafanya Mfuko wa Kinga ya Akiba na Amana kusimama imara.

Meza kuu


Washiriki wa vyama vya Akiba na Mikopo wakiwa katika kikao kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Josephat Kisamalala akiwasilisha taarifa ya Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar Es Salaam.

Washiriki wa vyama vya Akiba na Mikopo wakiwa katika kikao kikao kazi cha kujadili Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS kilichofanyika katika Ukumbi wa Ngome Holding Jijini Dar
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...