Na Karama Kenyunko Michuzi TV

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa bn kwa awamu ya tatu ya Udahili kwa wa waombaji wa Shahada ya Kwanza kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023 kuanzia leo Septemba 19 hadi 25, 2022

Katika taarifa iliyotolewa leo Septemba 19,2022 Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Charles Kihampa imesema kufunguliwa kwa dirisha hilo la Awamu ya Tatu kunatoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kudahiliwa au hawakuweza kuomba udahili katika Awamu mbili zilizopita kutumia nafasi hii ili kupata udahili.

Aidha, amewakumbusha waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza na wale wa Awamu ya Pili kujithibitisha katika chuo kimojawapo kuanzia sasa.

“Tume inaelekekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa shahada ya kwanza kuendelea kutangaza Programu ambazo bado zina nafasi. Aidha, waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya Tatu kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyo katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)” amesema Prof. Kihampa.

Pia Prof. Kihampa amewakumbusha waombaji wote wa udahili wa Shahada ya Kwanza kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika Chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika, na kwamba kwa wale ambao watapata changamoto ya kujithibitisha, Vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

Aidha TCU inawaasa wananchi kujiepusha na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu.

Pia TCU imeufahamisha Umma na wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa awamu ya pili ya Udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 imekamilika, na kwamba majina yawaombaji waliodahiliwa katika awamu ya pili yanatangazwa na vyuo husika.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...