Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amesema ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi , Mashirika ya Umma na Wadau wa michezo.
Amesema hayo leo Septemba 16, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali wa Mhe. Shaban Omari Shekilindi (Lushoto) aliyeuliza Je ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo katika Mji wa Lushoto.
Napenda kutumia nafasi hii, kuzikumbusha Halmashauri nchini ikiwemo Halmashauri ya Lushoto, kuzingatia matakwa ya Sera ya Michezo kwa kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu ya michezo" amesema Mhe.Gekul.
Mhe.Gekul ameeleza kuwa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 ibara 7 inaeleza jukumu la ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la watu wote na mazingira ya kuwekeza yameainishwa kwa uwazi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...