WIKI moja kabla ya kufanyika ya NMB Marathon ‘Mwendo wa Upendo,’ Benki ya NMB inayoandaa mbio hizo imetangaza wadhamini zaidi ya 20, ambao wameeleza siri ya uamuzi wa kukubali kudhamini kuwa ni kuguswa na wazo chanya la benki hiyo kuwakomboa kinamama nchini.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, aliwashukuru wadhamini hao kwa kusapoti mbio hizo na kurahisisha lengo la kukusanya Sh. Mil. 600 mwaka huu, hivyo kutoa nafasi mapato ya miaka miwili ijayo ya mbio hizo kuyaelekeza katika maeneo mengine yenye uhitaji.

Aidha, aliwataja Wadhamini Wakuu kuwa ni Sanlam Life Insurance na UAP Insurance (Executive), huku Jubilee General Insurance (ikiwa kategori ya Gold). Wadhamini wa kundi la Bronze ni pamoja na Alliance Life Assurance, Britam Insurance Tanzania, Reliance Insurance, ARiS Risk and Insurance Solutions na Metropolitan Life Insurance.

Wengine wa kundi hilo ni pamoja na, huku Toyota, TBL, Strategis, Serena Hotel, Azam, na Johari Rotana Hotel wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wengineo.

Katika kategori ya vyombo vya habari washirika, Kimori aliitaja EFM Radio, TV E, Mwananchi Communications Limited, IPP Media na Almasi Productions, orodha ilikamilishwa na Kampuni za SGA Security Tanzania, Gelato na Grano Coffee.

Lakini pia, wadhamini hao waliipongeza NMB kwa wazo chanya la kulikomboa kundi la kinamama wanaoshindwa kujitibu Fistula kutokana na gharama kubwa na kwamba kujitokeza kwao kuunga mkono jambo hilo, ni uthibitisho kwamba afya ya mama ni kipaumbele muhimu kwa jamii.

NMB Marathon 2022, zinazolenga kukusanya kiasi cha Sh. Mil. 600 za kusaidia matibabu ya kina mama wenye matatizo la Fistula wanaotibiwa kwenye Hospitali ya CCBRT, zitafanyika Oktoba 1 kwenye viwanja vya Leaders Club, Mgeni Rasmi akiwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...