Afisa Sheria, Bw. Abdulkarim Nzori kutoka Wakala wa Usajili na Biashara na Leseni (BRELA) akitoa ushauri kwa mzalishaji wa bidhaa za viungo vya chai, juu ya Usajili wa Alama za Biashara katika Maonesho ya Biashara ya Mara International Business Expo 2022, yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Mukendo mjini Musoma, mkoani Mara. BRELA inaendelea kuthoa huduma kwenye Maonesho hayo hadi tarehe 11 Septemba, 2022.
Maafisa kutoka Wakala wa Usajili na Biashara na Leseni (BRELA) wakihudumia wananchi wa mkoa wa Mara walipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Mara International Business Expo 2022, yanayofanyika viwanja vya Shule ya Msingi ya Mukendo, mjini Musoma. BRELA inawakaribisha wananchi wa Mara na mikoa jirani kufika katika maonesho na kupata ushauri na huduma za papo kwa papo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...