Katika Picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis Abdulla akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha katika hotel ya Mount Meru



Kutoka kulia ni Postamasta Mkuu Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo akifafanua jambo kiwa waandishi wa habari(Hawapo pichani )

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo ya siku tatu ya wakuu wa idara za usalama za posta zote za Afrika wakifuatilia kile kinachoendelea katika mafunzo



Na.Vero Ignatus,Arusha


Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la wa Posta Afrika,Shirika la Kimataifa la Posta Duniani imefadhili mafunzo ya siku tatu ya namna bora ya kuendesha huduma ambapo inajumuisha nchi karibia 50 za bara la Afrika na wapo washiriki zaidi ya 80

Akizungumza Mohamed Hamis Abdulla Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema kuwa lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa huduma wanazozitoa za Posta zinakuwa zenye viwango kwenye usalama na kujenga uaminifu kwa wateja wanaotumia huduma za posta

"Kikubwa kwenye mafunzo haya yanatutaka tufauli ambapo nchi itakuwa inapata cheti cha cha Kimataifa ambacho kinatambukika kwamba nchi yetu ya Tanzania ni salama kwa huduma zetu za posta''Alisema Naibu Katibu Mkuu

Abdullah amesema kuwa imawabidi kutoa mafunzo haya kwasababu dunia imebadikika na kuwa ya kidigitali zaidi kwani wale wati wetu walipo kwenue Shirika la Posta wanatakiwa waate uelewa kwamba sasahivi usalama upo kwenye teknolojia hivyo lazima iwajengee uwezo

Aidha ametoa Wito kwa watendaji wa Shirika la posta Tanzania, wachukulie mafunzo haya kwamba ni jambo la muhimu na la msingi japo kuwa watendaji ni wachache hao ndio watakaokwenda kuwafundisha watendaji wengine,ambapo baada ya mafunzo haya tutakua tumejenga uwezo mkubwa wa kikazi wa shirika la Posta nchini

Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo,amesema kuwa mafunzo haya siku tatu ya wakuu wa idara za usalama za posta zote za Afrika, yameandaliwa na Umoja wa Posta Duniani ili kuwajengea uwezo wa wakuu wa usalama wakuu wote wa posta za Afrika na kutengeneza mazingira wezeshi kwa kutafuta viwango vya ubora vya kiusalama katika huduma zote wanazozitoa

"Ifahamike kuwa huko mwanzo tulikuwa tukitoa huduma za kizamani, lakini baada ya mabadiliko ya kiteknolojia posta zote za Afrika zinapambana kubadilisha mifumo yake na uendeshaji wake wa kutoa huduma kwa wananchi tukiwemo Tanzania ,kwani siyo sisi pekee tunasafirisha vifurushi ndani na nje, biashara mtandao, huduma pamoja, posta kiganjani"

Amesema kuwa Posta kama wadau muhimu wameona ni muhimu kushiriki katika mafunzo hayo ili kuweza kujengewa uwezo kwa watalaam wao pamojaa na kujengewa mazingira wezeshi ya kuwahudumia wananchi

"Tunatarajia baada ya mafunzo haya Tanzania tutakuwa miongoni mwanchi za kwanza kabisa kupewa cheti hicho cha ubora wa usalama tumejiandaa kikamilifu vizuri kabisa ,timu ipo hapa kwaajili ya kupokea mafunzo na kufuata tarafibu zote za kupata cheti cha ubora wa usalama, kutoka Umoja wa Posta duniani" alisema Posta Masta Mkuu.

Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa huduma zote wanazitoa kwa wananchi zikiwemo huduma za kifedha, uwakala, usafirishaji, biashara mtandao zote wanazitia kwa njia salama kabisa kwa wananchi

Amesema mfumo wa posta mtandao wameitengeneza kwa kushirikiana na umfumo wa posta duniani umeinganishww na umekidhi viwango vyote vya usalama hivyo hakuna viti vyovyote hatari vinavyoonekana kwenye mfumo huo

"Lakini tunachokisema ni kwamba tunaitazama oostabyote kwanujumla wake katika huduma zote kuanzia mwanzo mpaka mwisho ndiyo maana wataalam wa umoja wa Posta kwaajili ya kufundisha Afrika yote ili kuhakikisha kwamba yeyote atakayefuzu atapata cheti cha kumtambua rasmi.Alisema

Caroline Kanuti, Mkurugenzi msaidizi huduma za posta idaravya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habar:i"Hawa wanaotoa mafunzo wanatoa vyeti, kuna nchi kadhaa za Afrika ambazo ni chache, mojawapo ikiwa Morocco ambayo tayari wamepata cheti kuthibitisha kwamba utoaji wa huduma za posta ni salama kimataifa, hivyo na sisi tumeanza mchakato huo tunapata mafunzo na tunakwenda kutekeleza yale tuliyoelekezwa namna gani ya kuboresha huduma za posta namna agani kushughukikia huduma na barua zao kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili tuweze kukidhi mahitaji ya kuwa na huduma salama

Caroline Kanuti:Tukishamaliza Mafunzo haya tutatuma tutayatumia kuboresha huduma kisha kuomba maombi waje watuangalie kama tumekidhi vigezo vya kupewa cheti cha kuwa naanhudima bora wa huduma za posta nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...