Namwandishi wetu,
MATUMIZI sahihi na salama ya huduma za mawasiliano ikiwa ni pamoja na usajili wa laini za simu za mkononi yatawawezesha wananchi wa Kigoma kufaidifursa zinazotokana na ukuaji wa kasi wa sekta ya mawasiliano na kujiendelezakimaisha.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, BwanaBoniface Shoo, amesema jana kwenye kampeni maalum ya matumizi sahihi yamtandao “KWEA KIDIJITALI” iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kalinzi Kigomakwamba usajili wa laini za simu ni hatuamuhimu inayomwezesha mtumiajikushiriki katika uchumi wa kidijitali.
Ameainisha huduma mbalimbali ambazo hazikuwepo miaka michache iliyopita na ambazo zimewezeshwa na matumizi ya simu za mkononi. Huduma hizo ni pamoja na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, kusoma kupitia intaneti, kununua bidhaa kupitia mtandao, kununuwa umeme, kulipia matibabu, kufuatilia matukio duniani na kushiriki katika kupasha wengine habari ama vile kupitia mitandao ya Kijamii. Kigoma inaongoza kwa kilimo cha michikichi ambayo inazalisha mafuta ya mawese hapa Nchini ambapo Bwana Shoo aliwataka wakazi wa mkoa huo kutumia mawasiliano, kutafuta masoko ya mazao yao.
Meneja wa TCRA Kanda ya Kati, Bwana Boniface Shoo, akitoa elimu kwa wadau-Kalinzi, Kigoma.
Kampeni hiyo, iliyofanyika kwenye gulio kijijini hapo ni sehemu ya mpango wa elimu kwa umma unaotekelezwa na TCRA chini ya kaulimbiu isemayo: “KWEA KIJIJITALI-Boresha Maisha yako,Tumia fursa zilizomo kwenye mfumo wa kidijiti kujiongezea kipato na kujendeleza kimaisha’’.
Elimu hii inalenga kuwawezesha wananchi na watumiaji kutumia fursa za mawasiliano na kuwa salama wanapotumia huduma na bidhaa kama vile simu za mkononi na huduma za intaneti.
Bwana Shoo amewataka wananchi wa Kigoma kutumia huduma za mawasiliano kwa kujiunga na mitandao ya simu za mkononi na kusajili laini zao za simu ili kuwawezesha kutumia huduma za pesa kupitia simu za mkononi na kupata huduma za intaneti na mitandao ya kijamii.
Kigoma ni mkoa wa 25 nchini katika usajili wa laini za simu, kwa mujibu wa takwimu za mwezi Juni 2022 zilizotolewa na TCRA. Jumla ya laini 1,257,318 zilikuwa zimesajiliwa Kigoma hadi Juni, kati ya laini milioni 56.2 zilizosajiliwa nchi nzima.
Usajili wa laini unafanyika kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho nakudhibitisha kwa alama za vidole. Watumiaji wanaweza kuhakiki usajili kwa kubofya *106# . Hii pia inawawezesha kubaini iwapo kuna laini zilizosajiliwa kwa namba zao za kitambulisho cha taifa bila ridhaa yao. Bw. Shoo aliwakumbusha wananchi kwamba Mawasiliano kati ya mtoa huduma na mtumiaji huduma za Mawasiliano ni mia moja tu, (100).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...