Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Samoei Ruto.

Aidha, Rais Samia atahudhuria uapisho huo wa Rais Ruto utakaofanyika jijini Nairobi kesho tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais Samia ataambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mhe. Harusi Said Suleiman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...