BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAKATI Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ukisomwa bungeni kwa mara ya kwanza,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Mwanza umekutana na viongozi wa serikali za wanafunzi,wataalamu wa TEHAMA,washauri na walezi wa wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Pia NHIF imewataka wanafunzi wa vyuo hivyo mkoani Mwanza kujisajili na kujiunga na mfuko huo ili kuwapunguzia wazazi na walezi gharama za matibabu, wasisubiri hadi waugue.
Akizungumza na wadau hao leo Meneja wa NHIF Mkoa wa Mwanza, Jalath Mushashu aliwataka wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu,kati,VETA na shule za sekondari ili kuepuka kukosa huduma wanapougua,wanajiunge na bima ya afya, wajisajili kabla ya muhula wa masomo,kupitia mifumo iliyopo vyuoni badala ya fomu na kufanya malipo baada ya kutengenezewa kidhibiti namba kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.

Alisema licha ya changamoto mfuko huo umeongeza idadi ya wanafunzi waliojiunga na bima ya afya kutoka 15,000 mwaka 2020/21 hadi kufikia 21,565 mwaka 2021/22,hivyo mwaka huu wanatarajia kuwasajili wengi kutokana wingi wa vyuo na mwamko uliopo.

“Tumekutana na viongozi wa serikali za wanafunzi kujadili changamoto za mwaka jana ili kuzifanyia kazi,uzoefu tuliopata mwaka 2021/22 ili kufikia matarajioa tutahakikisha wanafunzi wapata huduma kwa kuzingatia maelekezo ya serikali,kuwa na bima ya afya shiari ni lazima ili kupata huduma za matibabu wanapougua masomoni,” alisema Mushahu.

Alisema wanafunzi wakijiunga na NHIF watawapunguzia wazazi na walezi mzigo wa gharama za matibabu ingawa baadhi hupewa fedha na kuzitumia kwa mambo mengine, pia kuepuka kuchelewesha malipo ya wanachama vyuo viache kutumia mifumo ya zamani isiyo rafiki na NHIF.

Meneja huyo wa NHIF alivitaka vyuo vifunge mifumo madhubuti itakayoviwezesha kupata huduma mbalimbali zikiwemo za usajili wa wanafunzi,maboresho ya huduma mbalimbali za mfuko, malipo ya wanachama na taarifa zao.

Alisema ucheleweshaji malipo unasababisha wanufaika kuchelewa kupata kadi zao na kuzua malalamiko kwa mfuko huo wanapokosa huduma,nia ya NHIF kila mmoja awe na bima ya afya na kuonya watoa huduma wasio waaminifu wanaoshirikiana na wanafunzi kuwahudumia wasio wanachama watawajibika kisheria kwa kusababisha hasara na matumizi makubwa kwa wasiostahili na hilo halitavulimiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uanachama ya NHIF,Paul Bulolo alisema agenda ya serikali ya kila mwanafunzi kuwa na bima ya afya wanaiunga mkono,wameweka mkakati kuwafikia wananchi wote wawe na uhakika wa matibabu na kuwataka wamiliki wa vyuo kuwasajili watumishi wao kwa kuchangia asilimia sita ya mishahara.

“Uendelevu wa mfuko unategemea uchangiaji wa kundi kubwa la wananchi,watumishi wa umma,madhehebu ya dini na wanafunzi ingawa fedha ya mwanafunzi ni ngumu,hadi Juni 2021/22 idadi ya waliojiunga na vyuo ni kubwa lakini waliojiunga na NHIF ni wachache, hivyo tuna kazi kubwa ya kusajili wanafunzi wengi vyuoni,”alisema.

Naye mwakilishi wa Rais wa TAHILISO,Kamishna wa Afya,Alphoncina Mahundi,alisema afya ina umuhimu wa pekee,mwanafunzi asiyechangia NHIF,akitumia kadi ya matibabu isiyo yake ni kosa kisheria,hivyo serikali zote za wanafunzi zihamasishe kujiunga na NHIF pamoja na kutumia ofisi za mfuko kutatua changamoto.

“Serikali za wanafunzi mbali na kushirikiana kuibua changamoto na kuzitafutia ufumbuzi, zishirikiane na washauri wa wanafunzi kuondoa hili la kadi za bima kukaa muda mrefu bila kuchukuliwa na walengwa,kila mmoja awajibike kuhakikisha wanafunzi wanajiunga na mfuko wa NHIF,”alisema.

Aidha mmoja wa wadau hao Liberatus Ndegeulaya, alishauri wanafunzi wanaotengenezewa kidhiditi namba lakini hawalipii kwa madai hawaugui, uwekwe mfumo wa kuwadhibiti kuhakikisha wanalipa,pia wenye bima binafsi za afya uandaliwe utaratibu waunganishwe na NHIF.
Kwa mujibu wa takwimu hadi Juni 2021 NHIF ilikuwa na wanachama 4,403,581 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote ambapo asilimia 69 ni watumishi wa umma na asilimia 31 wananchi wanaojichangia kwa hiari.

Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoa wa Mwanza, Jalath Mushashu akizungumza na viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu, kati na ufundi leo jijini Mwanza.

Mkuu wa Idara ya Uanachama NHIF Mwanza, Paul Bulolo akitoa mada kuhusu maboresho ya huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo, kwa wanachama wakiwemo viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu,vya kati na vya ufundi leo jijini hapa.

Viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu, vya kati na vya ufundi wakiwemo washauri wa wanafunzi,walezi, walimu na wataalamu wa TEHEMA wakifuatilia mada mbalimbali leo walikupokuta na uongozi wa NHIF Mwanza kujalidi changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa mkutano wa wadau wa mfuko wa NHIF,ambaye pia ni Mkufunzi wa IT,aliyetambulikakwa jina moja la Swai akizungumza na viongozi wa serikali za vyuo vikuu, vya kati na ufundi, wakiwemo washauri wa wanafunzi na walezi (hawapo pichani) leo.Picha zote na Baltazar mashak

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...