Na Mwandishi wetu.

WATANZANIA wameshauriwa kuendelea kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu ili kujiongezea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa big bad wolf sharjah mohamed noor hersi wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu uuzaji wa vitabu vya big bad wolf tanzania 2022, unaotarajiwa kufanyika kuanzia septemba 8 hadi 18 mwaka huu.

" Tamaduni ya kusoma imepungua sana duniani sasa hvi, hivo sisi tunajitahidi sana kufanya hivi ili tuweze kurudisha ile hali ya watanzania kupenda kusoma "

amesema lengo la kuanzishwa mpango  wa uuzaji wa vitabu ni kuwajengea mazoea wananchi na kupelekea kuwa na kizazi chenye utamaduni wa kusoma vitabu duniani bila kujali kiwango chao cha kipato.

 Nae mtendaji wa taasisi ya big bad wolf Ndg. sharjah andrwe amesema  vitabu vitakavyouzwa ni vitabu vya picha, shughuli kupaka rangi na vitabu shiriki.
                                         
Tanzania inakuwa nchi ya kwanza barani afrika kupitiwa na mpango huo ambao umeshapita katika nchi 13 duniani na vitabu hivyo vimeandikwa katika lugha ya kiingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...