Na Eleuteri Mangi, WUSM
BALOZI wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko amesema Watanzania wamehamasika na wamekuja kwa wingi katika Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika kuanzia Septemba 4-12, 2022 nchini Burundi.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly amesema hayo Septemba 06, 2022 mara baada ya kutembelea mabanda ya wajasiriamali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioleta bidha zao kwenye hilo.
Nimemaliza kutembelea mabanda ya Tanzania na nchi nyingine, nimeona hamasha kubwa sana Watanzania waekuja kwa wingi, watu mbalimbali wameleta bidhaa za Sanaa, chakula na kwa sababu Burundi wanapenda sana bidhaa za chakula kutoka Tanzania. Nimeona jinsi wanavyochangamkia mchele, dagaa, viungo vya chakula, mafuta, nguo batiki, mapambo ya mwili na picha za Tingatinga, kwa kweli maonesho yamefana” amesema Mhe. Balozi Dkt. Jilly.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana pamoja na watanzania ambao wamekuja kweny tamasha hilo kwa kuwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo Wtanzania waishio nchini Burundi, jamii ya kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, wafanyakazi wa mashirika pamoja na kikanda na kuwahimiza kutembelea mabanda yote ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masariki (EAC).
Pamoja na maonesho hayo ya Sanaa na Utamaduni, mada mbalimbali ziliwasilishwa tamasha hilo kiwemo jukumu la teknolojia ya kisasa kwa kutumia utamaduni, tasnia ya sanaa na utalii, ushiriki wa vijana katika shughuli za sanaa katika jumuiya ya EAC pamoja na matokeo ya uvumbuzi katika sanaa na utamaduni.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (aliyevaa miwani) akitembelea mabanda ya wajasiriamali ya Watanzania alipotembelea mabanda hayo wakati wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea nchini Burundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...