Na.Khadija Seif Michuzi Tv

WAZAZI wametakiwa kujipanga/kuzaa watoto kwa kufuata njia za uzazi wa mpango ikiwemo vipandikizi, sindano na vidonge Ili waweze kuzaa watoto wenye afya nzuri na waweze kuwahudumia kwa kuwapa malezi mazuri ikiwemo elimu bora na matunzo mazuri kwa mustakabali wa maisha yao.


Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo wakati alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya uzazi wa mpango yalioandaliwa na DKT Tanzania yaliofanyika katika hospitali ya Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam sambamba na kutoa zawadi mbalimbali kwa wamama waliojifungua.

Amesema kuwa, endapo wazazi watatumia njia salama za uzazi wa mpango wataweza kuzaa watoto wazuri wenye afya ambao watajenga jamii bora na nchi iliyoimara, hivyo amewataka wazazi wote wawili waone umuhimu wa kuzaa kwa kutumia uzazi wa mpango.

Kwa upande wake, Meneja Masoko kutoka DKT Tanzania Deogratius Kithama amesema kuwa lengo la kutoa zawadi mbalimbali kwa wamama waliojifungua ni miongoni mwa hamasa ya wazazi kuweza kutumia njia za uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Muuguzi kutoka hospital hiyo, Elizabeth Maige amesema kuwa wamama wengi wanaofika katika hospital hiyo kwa ajili ya kujiunga na uzazzi wa mpango wanatumia njia ya kipandikizi cha miaka 3 ambapo wanadai hiyo ni rahisi kuliko ya vidonge.

Nao, wazazi waliopatiwa zawadi hizo wameshukuru na kupongezwa kampuni hiyo kwa kuwajali kwa kuwapatia bidhaa hizo ikiwa ni njia ya kuwahamasisha watumie uzazi wa mpango.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo wakati alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya uzazi wa mpango yalioandaliwa na DKT Tanzania yaliofanyika katika hospitali ya Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam

Meneja Masoko kutoka DKT Tanzania Deogratius Kithama akizungumza na wamama ambapo Kampuni ya DKT imetoa zawadi ya njia za uzazi wa Mpango Kwa wamama waliojifungua katika hospital ya Mbagala Rangi tatu Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...