WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe.

Taratibu za kutoa heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan. Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.

Bw. Abe ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

Akiwa Japan, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani Waziri Mkuu, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es salaam. Kushoto ni mkewe mary na wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...