Na.WAF, Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Viongozi wa Mashirika ya Kimataifa na Wadau wa maendeleo nchini na kujadiliana njia za mbalimbali za utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola uliopo nchi jirani ya Uganda.

Kikao hicho kimefanyika leo Septemba 29, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amepongeza jitihada zinazofanywa na wadau hao wa Maendeleo katika mapambano dhidi ya Magonjwa pamoja na kutoa ushauri kwa Serikali njia na namna ya kukabiliana na magonjwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Aidha, katika kikao hicho Waziri Ummy amepokea msaada wa vifaa kinga(PPE) kwa ajili ya watoa huduma za afya Vyenye thamani Zaidi ya Bililioni moja kutoka Serikali ya Ireland.

Akiongea katika kikao hicho Dkt Zabron Yoti, Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini ameihakikishia Serikali kwamba WHO ipo tayari kukabiliana na Magonjwa ya milipuko na itaendela kuwa mshirika wa karibu zaidi kwa kutoa msaada wa kitaaluma na rasilimali katika kusaidia Serikali kupambana na magonjwa Ukiwemo Ugonjwa wa Ebola ulipo nchi jirani.

Katika kikao hicho pia viongozi hao wametoa mawazo yao juu ya kukabiliana na ugonjwa huu wa Ebola na tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini na hata ukiingia wamejipanga kwa kukabiliana nao.

Kwa upande wao wadau hao wa maendeleo wakizungumza, wameipongeza Serikali katika jitihada inazozifanya kuhamasisha na kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga na Magonjwa ya milipuko pindi yanapotokea na kuanza kupambana nayo.












 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...