· CBE yakamilisha majengo yake kampasi ya Mbeya
· Waziri Mkuu kuzindua kampasi ya CBE Mbeya Oktoba 8
Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimesema mwitikio wa wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika kampasi yake mkoani Mbeya imekuwa ya kutia moyo.
Hayo yalisemwa jana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Profesa Emmanuel Mjema, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilele cha harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii jijini Mbeya.
“Tunashukuru mwitikio umekuwa mzuri na mkubwa watu wamejitoa kuendelea kuchangia na wengine wamethibitisha kwamba watakuja Mbeya kushiriki harambee hivyo tunawashukuru na kuwataka wengine waendelee kuchangia,” alisema
Vile vile, alisema (CBE), imekamilisha ujenzi wa kampasi yake mkoani Mbeya yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,000 na mpaka sasa kimeshachukua wanafunzi 1,000 tayari kwa kuanza masomo.
Alisema majengo ya chuo hicho yanatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 8 mwaka huu jijini Mbeya na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Alisema majengo yaliyokamilika ni ya utawala, kumbi za mihadhara, maktaba na ofisi za wafanyakazi.
Profesa Mjema alisema mpaka kukamilika kwake majengo hayo yamegharimu Sh bilioni 1.46 ambazo zimetokana na mapato ya ndani.
“Napenda kutoa taarifa kwamba ujenzi umekamilika ambapo kwa sasa mazingira ni mazuri kwani miundombinu mipya na ya kisasa inakifanya chuo kutoa huduma kwa ufanisi na tunaomba wadau wajitokeze kuchangia tujenge mabweni ya wasichana,” alisema Profesa Mjema
Alisema wanafunzi wakike wanaishi kwenye mazingira magumu kwani wengi wao wanaanza chuo wakiwa na umri mdogo na ndiyosababu wametoa kipaumbele kwao kujengewa bweni.
Profesa Mjema alisema kilele cha harambee ya kujenga mabweni ya wasichana itafanyika Jumamosi ya tarehe 24 mwezi huu jijini Mbeya na mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge ambaye ndiye mlezi wake, Dk. Tulia Ackson.
Alisema chuo kimefanya juhudi za kuwafikia wadau mbalimbali zikiwemo taasisi namashirika ya serkali na yasiyo ya kiserikali pamoja na sekta binafsi kuchangia ujenzi huo.
Vilevile, alisema chuo kimeweza kufikisha jambo hilo kwa wabunge kwani pia ni wadau muhimu wa maendeleo ya Elimu nchini.
“Tunawaomba wadau wotewenye mapenzi mema na maendeleo walipo ndani na nje kutushika mkono kwa kuchangiachochote ili tuweze kukamilisha harambee pia tukimuunga mkono mlezi wa Kampasi ya CBE Mbeya, Dk. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania, ambaye niMbunge wa Mbeya Mjini,” alisema.
Aliwashukuru wadau ambao tayari wamechangia nawengine kutoa ahadi zao na kuwataka wanaoweza kuchangia kutumia akaunti ya NMB namba 20601100030 au MPESA 977992.
CBE ina kampasi tatu za Mbeya, Mwanza na Dodoma na yanne ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi wa 11 baada ya chuo hicho kukabidhiwa eneo na Serikali ya Zanzibar.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...