Na Shamimu Nyaki- India

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) kwa ushindi wa magoli mawili kwa Moja dhidi ya Ufaransa.

Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa Oktoba 15, 2022 Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa, India imeipandisha Tanzania hadi nafasi ya pili nyuma ya Japan na mbele ya Canada na Ufaransa katika kundi hilo.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inatoa mchango mkubwa kwa timu zinazowakilisha vyema  nchi, na ndio maana hata nyie Serengeti Girls Serikali ipo hapa nanyi kuhakikisha inawaunga mkono mfanye vizuri" amesema Mhe. Gekul

Kwa upande wake Kocha wa timu Bakari Shime, amesema vijana wanaendelea kuimarika na kusahihisha makosa ya Mechi ya kwanza dhidi ya Japan ambayo leo umeleta matokeo mazuri.

" Kesho tutaelekea Mumbai na tukifika tutafanya mazoezi kwa ajili ya mchezo na Canada ambao tukishinda tunasonga mbele" amesema Kocha Shime.

Tanzania ipo katika kundi D pamoja na Japan, Ufaransa na Canada.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...