Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SHIRIKA la Can Tanzania ambalo linajihusisha na makabiliano ya mabadiliko ya tabaanchi na usimamizi wa mazingira limesema umefika kuhakikisha taarifa za utabiri wa muelekeo wa hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) ziwe zinatolewa mahususi kwa eneo dogokadri inavyowezekana.

Ikiwezekana utabiri wa TMA uwe unatolewa hata katika Kata au Kijiji kwani tayari katika nchi nyingine wamefikia mpaka mitaa kwa hiyo hizo zinakuwa taarifa ambazo zinategemewa na zinatoa taarifa halisi ya nini kifanyike badala ya kuendelea kuwa na taarifa za utabiri ambao unazungumzia muelekeo kwa kuangalia Kanda.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 13, 2022 na Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira Can Tazanzania Dk.Sixbert Mwanga wakati wa kikao cha wadau wa matumizi ya utabiri wa hali ya hewa waliokutana kwa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa kutumia lugha rahisi na sahihi kuhusu taarifa za utabiri wa hali ya hewa.

Dk.Mwanga amesema kunakupokuwa na utabiri wa hali ya hewa unaogusa eneo dogo ni rahisi kwa wananchi wa eneo husika kufahamu wafanye nini kuhakikisha wanatumia utabiri huo katika kufanya shughuli zao za kila siku zikiwemo za kilimo.

“Kwa mfano unatoa utabiri wa muelekeo wa mvua kwa kutumia ukanda wa Pwani ambao unaanzia kusini mpaka Tanga , mle katikati kuna Lindi, Dar es Salaam ambapo mvua inaweza kunyesha.Mvua inaweza Mbagala na isinyeshe Kinondoni lindi lakini mtu wa Kinondoni akawa ameaanda shamba lake na kupata hasara.Hivyo ni muhimu kuwa na taariga zinazogusa eneo dogo,”amesema Dk.Mwanga.

Aidha amesema pamoja na kutolewa kwa taarifa za utabiri wa hali ya hewa bado wanahisi hazifiki kwa mtumiaji wa mwisho.“Kwanini? Kwasababu taarifa inapotoka za utabiri wa hali ya hewa kwa sasa hivi kwa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania zinapitia njia kuu mbili.

“Njia ya kwanza ni televisheni ambayo sina sensa ni watu wangapi wanatumia na wanaweza kuwa na umeme. Na wengi wako vijijini ni wakulima , na wanaweza wasipate hizi taarifa, nyingine ni redio , kuna watu wangapi wanakuwa na redio wakati wote , kwa hiyo bado tunahitaji maofisa ugani kuhakkisha wanapata hizo taarifa na tena tunawapa taarifa zao kama ni Korogwe unampa taarifa ya Korogwe. “Sio unampa taarifa ya ukanda mzima ambayo yeye haitamsaidia.

Pia bado tunadhani kuna ugumu wa kuzielewa tabiri ya hali ya hewa, unaposema mvua zitakuwa chini ya wastani unamaanisha nini ,mkulima afanye nini, mfugaji afanye nini, mvuvi afanye nini , mwendesha bodaboda afanye nini, “amesema.

Ameongeza kwa hiyo wadau hao wamekutana kwa ajili ya kujaribu kujenga uelewa ili mwisho wa siku wanakuwa na uelewa wa pamoja.“Siku Mamlaka ya Hali ya Hewa inaposema mvua itanyesha juu ya wastani upande wa Pangani kwa hiyo mtu wa Pangani ajue maana yake ni nini na anatakiwa afanye nini,kama anawajibika kuhama kutoka kwenye mabonde kwenda juu ya mlima ajiandae.

Kuhusu taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa inapokuwa imetoka moja kwa moja bila kugusa eneo husika zisinyenyeshe.” Mwisho kwa maana haikutengenezwa katika mfumo wa kutoa taarifa katika eneo dogo amesema utabiri huo unaweza kuleta changamoto kwa wananchi.

Amefafanua maana utabiri ule unaweza sema mvua inaweza kunyesha Kanda ya Ziwa lakini kanda ya ziwa ina mikoa mingi kwa hiyo utakuta mvua inanyesha Karagwe na haikunyesha labda Sengerema. “Lakini mtu wa Sengerema katika utabiri huo wa jumla ulimwambia aandae shamba na mvua zitaanza kunyesha kwa hiyo ukakuta yeye amepata hasara amenunua mbegu amepanda amefanya kila kitu halafu mvua.
Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira Can Tazanzania Dk.Sixbert Mwanga (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa matumizi ya utabiri wa hali ya hewa kutoka taasisi za elimu ya juu,Wizara, Taasisi za Umma na binafsi, pamoja na makundi ya watu mbalimbali baada ya kumalizika kwamajadiliano ya kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa kutumia lugha rahisi na sahihikuhusu taarifa za utabiri wa hali ya hewa.Profesa Henry Mahoo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) wa pili kulia akifafanua jambo kwa wadau hao.Baadhi ya wadau wakijadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu taarifa za utabiri wa muelekeo wa hali ya mvua.



Meneja Ptogramu wa Shirika la Can Tanzania Nuru Nguya(kulia aliyevaa hijabu) akitoa ufafanuzi wakati wa majadiliano ya wadau wa matumizi ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa
Mratibu wa Sera na Utafiti kutoka Can Tanzania Mkombozi Joannes(kushoto) akijadiliana jambo na moja ya wadau waliohudhuria mkutano huo.

Wadau wa matumizi ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa wakiendelea na majadiliano.Wadau wakiendelea na majadiliano kuhusu matumizi sahihi ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na TMA.
Meneja Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Isack Yonah(kulia) akijadiliana jambo na Ofisa Sera na Mawasiliano wa Shirika la Can Tanzania Lucas Horndach

Mmoja ya wadau wa mazingira kutoka Chalinze mkoani Pwani ambaye anajihusisha na kilimo pamoja na ufugaji Lucas Sultan (kulia) akichangia jambo wakati wa majadiliano yaliyokuwa yakiendelea.

Baaadhi ya wadau wakiendelea kujadiliana wakati wa mkutano huo ukiendelea ambapo waliwekwa kwenye makundi mbalimbali kwa ajili ya kuchambua taarifa za muelekeo wa utabiri wa mvua zinatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...