Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia wakishikana mkono na wakandarasi baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano ya Chuo hicho, hafla ambayo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akisaini Mkataba na wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa majengo matano ya Chuo hicho, hafla ambayo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James akizungumza akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu) Prof. Carolyne Nombo akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam


Na Mwandishi wetu, Michuzi TV
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeingia mkataba na wakandarasi kujenga majengo matano ya Chuo hicho wenye thamani ya Bilioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na benki ya Dunia na kusimamiwa na Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia.

Aidha Serikali imewaamuru wakandarasi waliopewa tenda hiyo kujenga majengo bora na siyo bora majengo kulingana na thamani ya pesa na kukabidhi majengo hayo kwa wakati kama makubaliano ya mkataba yanavyotaka

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji saini ilitofanyika leo Oktoba 28,2022 katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu) Prof. Carolyne Nombo amesema, serikali itasimamia mradi huo mpaka pale itakapohakikisha malengo yake yanafikiwa.

Ninawaomba wakandarasi, mkafanye kazi kwa bidii na uweledi ili kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa muda uliopangwa yaani miezi 12 kwani majengo haya ni muhimu kwa ustawi mafunzo yanayotolewa NIT hivyo naomba ujenzi uanze kwa kasi huku mkizingatia taratibu zote za kisheria na za kiufundi ili kukamilisha kazi hii kwa ubora na kwa muda mfupi inavyotarajiwa" amesema Profesa Nombo

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa amesema chuo hicho kimeanzisha kituo cha umahiri katika taaluma ya anga na masuala yote ya usafirishaji ambapo tayari NIT imefika asilimia 75 ya utekelezaji.

Amesema kuwa mkataba wa ujenzi uliosainiwa unathamani ya shilingi Bilioni 21 ambapo ujenzi huo huo utafanywa kwa mwaka mmoja.

Profesha Mganilwa pia ameyataja mafanikio ya kituo hicho kuwa mbali na kutoa elimu bora pia kimetengeneza miongozi na sera 15 kukisaidia chuo kuingia makubaliano na mashirika na wadau mbalimbali wa usafirishaji.

Pia kimetengeneza mitaala mipya 11 ya muda mrefu na kuongeza kuwa hakuna chuo kingine kinachofundisha air Transport Managment au Railway Transport Management zaidi ya NIT.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James amesisitiza wakandarasi waliopewa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati kama ambavyo serikali inatarajia.

Amesema kuwa kwa upande wake kama Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambapo chuo hicho kimo wilayani humo atatoa ushirikiano kuhakikisha ujenzi unakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...