Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ludigija, amepiga marufuku kwa wafanyabiashara ndogo 'Machinga', kufanya biashara chini ya transifoma za umeme au laini za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Ludigija alitoa katazo hilo, Dar es Salaam, leo Oktoba 7,2022 alipokagua miundombimu ya TANESCO, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mkoa wa Ilala Kitanesco.

Alisema kufanyabiashara karibu na miundombinu hiyo kunaweza kuhatarisha maisha yao, pia wanaweza kusababisha upetevu wa udhalisaji wa umeme endapo itatokea hitirafu.

"Nitoe tahadhari kwamba wakati mafundi wa shirika hilo wanafanyakazi ya kubadilisha nyaya bila kukata umeme, kwani kuna umeme mkubwa umepita juu, hivyo wafanyabiashara wasitishe shughuli zao", alisema.

Pia Ludigija ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara kujiunganishia umeme kwa kutumia vishoka.

Alisema TANESCO haiwezi kumuunganishia mfanyabiashara umeme katika eneo ambalo laini kubwa ya umeme imepita.

Ludigija alisema kila mtu anayetaka kuunganishiwa umeme afike katika ofisi za Tanesco, pia ofisi hizo zinafanya kazi muda wote.

Alisema shirika hilo limeboresha mifumo yake, ambapo mteja anaweza kuomba kuunganishiwa umeme kwa kutumia mfumo wa kidigitali ikahudumiwa haraka ukiwa nyumbani.

Pia amelipongeza shirika hilo kwa kuimalisha huduma zake, baada Rais Samia Suluhu Hassan, kutoa zaidi ya Sh. bilioni 2.7, ambazo zimetumika kubadilisha transifoma mbalimbali zaidi ya 100.

"TANESCO imefanya kazi kubwa kulingana na fedha walizopewa na Rais Samia, kwasasa sijapokea malalamiko kutoka kwa wananchi, endeleeni kufanya kazi hivyo hivyo ili wananchi waendelee kupata huduma hii umeme kwani ni muhimu.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'ilabuzu Ludigija akizungumza na watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wananchi kutunza miundombinu ya Shirika hilo.

Matukio mbalimbali katika picha wakati Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'ilabuzu Ludigija alipotembelea Ofisi za TANESCO Ilala leo Oktoba 7,2022Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'ilabuzu Ludigija akifafanua jambo alipotembelea kuangalia kuangalia miundombinu ya TANESCO wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Baadhi ya watumishi wa TANESCO Mkoa wa Kitanesco Ilala wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'ilabuzu Ludigija ( hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...