Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha amesema moja ya mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii ni kuhakikisha migongano baina ya binadamu na wanyamapori hasa kwenye maeneo ya pembezoni mwa Hifadhi inapungua kwa kiasi kikubwa.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Oktoba, 2022 wakati wa kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma kilichozikutanisha timu ya Watalaam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ),

Hatua hiyo inakuja kufuatia Serikali ya Tanzania kupokea Euro milioni 6 sawa na shilingi bilioni 13.2 kutoka Shirika la Ujerumani la GIZ kwa ajili ya mradi wa kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyamapori katika mfumo wa Ikolojia Selous Niassa

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt.Msuha amesema Serikali imekuwa ikifanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kuwa Wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Hifadhi hawaathiriwi na wanyamapori hao badala yake wanatumia maeneo hayo katika kujinufaisha kiuchumi

Ameeleza kuwa moja ya mikakati ambayo Serikali imekuwa ikifanya ili kukabiliana na wanyamapori hao ni kuwavisha vifaa maalum vya utambuzi kwa wanyamapori viongozi pamoja na kuwajengea uwezo wananchi katika kukabiliana na wanayamapori wakali na waharibifu.

Naye, Mkurugenzi wa GIZ nchini Tanzania, Dkt. Mike Folke amesema Serikali ya Ujerumani imelazimika kutoa fedha hizo kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika Uhifadhi wa Wanyamapori

‘’Watanzania wanapenda sana kuhifadhi wanyamapori hivyo kama migongano kati ya binadamu na wanyamapori hataidhibitiwa Watanzania hawa wanaowapenda wanyama hao wataanza kuwachukia wanyama hao’’ alisistiza Dkt. Mike Folke

Mradi huo wa kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu utakaofanyika katika baadhi ya Wilaya za Ruvuma zenye changamoto za wanyama unatarajiwa kuanza hivi karibuni na utadumu kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu (2022-2025)
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha akizungumza wakati wa kikao cha  kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali  na waharibifu  kilichofanyika leo  Jijini Dodoma kilichozikutanisha timu ya  Watalaam kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ)
 Kikao cha  timu ya  Watalaam kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ), kilichokutana leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mkoani Ruvuma

Mkurugenzi Msaidizi wa Wanyamapori, Dkt. Fortunata Msoffe akifurahi jambo na Kiongozi Mkuu wa Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani  (GIZ)  Bruggemann  kikao mara baada ya kikao kilichowakutanisha  leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mkoani Ruvuma
Mkurugenzi wa Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akipeana na  Joheness  Schweneberg kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani  (GIZ)   mara baada ya kikao cha timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ),katika kikao kilichowakutanisha  leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mkoani Ruvuma
Mkurugenzi wa Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha (katikati)  akiwa kwenye picha ya pamoja na  Watalaam kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ), mara baada ya kiko kilichowakutanisha  leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutambulisha mradi wa kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mkoani Ruvuma

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...