WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameshiriki Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano katika msuala ya Ulinzi na Usalama (JPCDS) baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa Joachim Chisano, Maputo nchini Msumbiji. Mheshimiwa Waziri akiwa Mwenyekiti Mwenza wa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Mheshimiwa Cristovao Chume.

Mkutano huu unafanyika kwa mara ya nne sasa, Mkutano wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam, Tanzania tarehe 04 - 06 Februari, 2011 ambapo Tume hii ilianzishwa rasmi.

Mkutano huo umefanyika kwa ngazi tatu, ambapo ulianza kwa kutanguliwa na ngazi ya wataalamu , ukifuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa mawairi wenye dhamana ya masuala ya ulinzi na Usalama wa mataifa haya mawili.

Pamoja na mambo mengine vikao vya ngazi zote vilijadili ushirikiano kuhusu masuala ya kiulinzi, na hatimaye kutoa fursa kwa Mawaziri hawa wawili, kusaini mikataba itakayowezesha kutekelezwa kwa Hati ya Makubaliano kuhusu ushirikiano kupitia sekta ya Ulinzi na usalama, uliosainiwa kwa pamoja tarehe 21 Septemba, 2022 na Mawaziri wa pande zote mbili. Utiaji saini huo, ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu, aliyoifanya Rais Samia nchini Msumbiji hivi karibuni.

Mbali na Mheshimwa Dkt. Stergomena, ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha pia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz, Mheshimiwa Angelina Sylvester Lubala Mabula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, viongozi wandamizi wakuu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mataifa yote mawili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...