Waliofariki kwa ajali za bodaboda Januari hadi Septemba watu 211, majeruhi 212

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMANDA wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu kulikuwa na ajali za pikipiki 296 zilizosababisha vifo vya watu 211 na majeruhi 212.

Kamanda Mutafungwa amesema hayo leo Oktoba 15,2022 wakati uzinduzi wa maeneo salama ya kusubiria(Buffer Zone) kwa waendesha pikipiki hasa wanapofika katika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama, michoro na taa za kuongozea watumiahi wa barabara,magari, pikipiki na watembea kwa miguua.

“Tunaishukuru Serikali kupitia TANROADS kuona umuhimu wa kuwa na maeneo salama kwa kundi hili la watumiaji wa barabara .Niwashukuru wadau wetu wa usalama barabarani TBL kwa kuona umuhimu wa kushiriki kwa ufadhili wa hali na mali.

“Katika utoaji elimu ya usalama barabarani  na kutumia sehemu ya faida yao kwa manufaa ya watumiaji wa barabara hasa waendesha pikipiki,”amesema Kamanda Mutafungwa na kuongeza katika Wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Arusha TBL kwa kushirikiana na Polisi walizindua program hiyo kwa watumiaji wa barabara hasa waendesha bodaboda.

Ameongeza katika ushirika ule ule wanakwenda kuzindua mpango huo jijini Dar es Salaam na kutoa ombi kwa mikoa mingine wafanye hivyo kwa manufaa na usalama wa watumiaji wa barabara.“Uzinduzi wa maeneo ya Buffer Zone kwa waendesha pikipiki hasa wanapofika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama, michoro na taa za kuongozea watumiaji wa bararabara. 

"Ni  muhimu sana katika dhana nzima ya usalama barabarani kwa kulinda maisha ya watu na mali zao watumiapo barabara.Aidha tumekuwa wakishuhudia ajali nyingi zikitokea katika maeneo hayo hasa kwa kuwa madereva wa pikipiki wanakosa elimu na maarifa ya kutosha kuepusha ajali za barabarani ama kwasababu ya kutojua au kupuuzia na kudharau kwa kutotii sheria za barabarani."

Kamanda Mutafungwa amesema katika makundi ya watumiaji wa barabara , waendesha pikipiki maarufu bodaboda ni kundi kubwa ambalo linashiriki kutoa huduma ya usafiri kwa watu wengi , hivyo linapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabara.

Ameongeza kwa Jeshi la Polisi, kikosi cha Usalama Barabara litaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kundi hilo kubwa linafikiwa kwa elimu ya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuokoa maisha ya watu na mali zao.Aidha ametoa rai kwa waendesha bodaboda kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kijinai kwani baadhi yao wanapojihusisha wanaharibu sifa ya biashara ya kusafirisha abiria kwa bodaboda. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Jose Moran alisema, “Kila maisha yana thamani isiyopimika. Kila hasara inawakilisha uwezo ambao haujatimizwa. Inasikitisha sana kupoteza watu wengi huku ukizingatia kuwa mara nyingi ajali hizi zinaweza kuzuilika.

Alama za kanda za bafa (Buffer zones)  ni kuongoza kwenye makutano ya barabara yenye shughuli nyingi, ambazo zinadhibitiwa na taa za trafiki, ambazo zitatenganisha pikipiki na magari mengine. Haya yanajiri baada ya uchanganuzi unaoonyesha ajali nyingi zinazotokea kwenye makutano  kutokana na mwingiliano wa fujo wa pikipiki na magari.

Kama uthibitisho wa dhana, maeneo ya buffer yaliyoanzishwa nchini Brazili yalipunguza ajali zinazohusisha pikipiki kwa 25% katika mwaka mmoja. Alisema MoranKwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema leo wamekuwa uzinduzi wa wa kuweka  alama za barabarani hasa kwa waendesha bodaboda ambao ni usafiiri muhimu katika jiji la Dar es Salaam.

“Mimi kama msimamizi wa shughuli za Serikali jambo hili ni nzuri ambalo linafanywa na wenzetu wa Polisi pamoja na TBL lakini likishirikisha waendesha bodaboda na lengo kubwa ni kuhakikisha kunakuwa na usalama kwa watumiaji wote wa barabara.ni muhimu kwa kila mtumiaji wa barabara kuheshimu alama zilizowekwa.

“Kwasababu lengo kubwa ni kuhakikisha kila mtumiaji wa barabara anakuwa salama, hapa mjini tumekuwa tukipokea changamoto nyingi hasa matukio ya ajali ambayo yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya Taifa kwa vijana , abiria kupata ulemavu. Hivyo tunapongeza jitihada hizi,”amesema Ludigija.

Ameongeza matarajio yake ni kuona alama hizo za waendesha pikipiki zinakuwa katika barabara zote za TANROADS, TARURA kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania na mwito wake kwa waendesha bodaboda kuheshimu alama za barabara ili kuhakikisha wanaepukana na ajali wao na abiria wanawaowabeba.Kamanda wa Polisi, kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa(wa pili kulia),Mkuu wa

Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija(wa watatu kulia) Mkurugenzi Mkuu wa TBL Jose Moran (wa kwanza
kulia) wakiwa pamoja na wadau wengine wakati wakizindua maeneo ya kusubiria(Buffer Zone) kwa
waendesha bodaboda katika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama, michoro na taa za
kuongozea watumiaji wa barabara.Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa kwenye pikipiki zao kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa alama za usalama za kurubiria(Buffer Zone) ambazo ni maalumu kwa waendesha bodaboda wanapokuwa katika maeneo ya makutano ya barabara , lengo ni kuhakikisha wanakuwa salama kwa kusimama katika alama maalumu.Baadhi ya michoro maalumu ambayo itatumiwa na waendesha bodaboda pindi wanapofika kwenye makutano ya barabara.Alama hizo za michoro zimezinduliwa leo Oktoba 15,2022 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi, kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija, Meneja wa Programu wa Barabara Kuu za TANROADS Dk.Christina Kayoza pamoja na wadau wengine.Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua maeneo salama ya kusubiria(Buffer Zone) kwa waendesha bodaboda hasa wanapofika katika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama, michoro na taa za kuongoza watumiaji wa barabara.Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija(wa tatu kulia) akiwa na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa maeneo salama ya kusubiria(Buffer Zone) kwa waendesha bodaboda wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwaombea watu wote ambao wamepoteza maisha kwa ajali za barabara hasa zinazotokana na bodaboda kabla ya kuzinduliwa kwa buffer Zone kwa waendesha pikipiki wanapofika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama , michoro na taa.Kamanda wa Polisi, kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Wilbroad Mutafungwa(katikati) akiwa na maofisa wa kikosi hicho, maofisa kutoka TBL na TANROADS pamoja na waendesha bodaboda(waliosimama nyuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa alama za barabarani za maeneo salama ya kusubiria(Buffer Zone) kwa waendesha bodaboda jijini Dar es salaam.Kamanda wa Polisi ,Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TANROADS, TBL, Mkuu wa wilaya ya Ilala pamoja na maofisa wa jeshi hilo kikosi baada ya kuzinduliwa kwa alama za maeneo salama ya kusubiria kwa waendesha bodaboda wanapokuwa maeneo ya makutano ya barabara.Mkurugenzi Mkuu wa TBl Jose Moran(katikati) akifurahia jambo wakati Kamanda Wilbroad Mutafungwa(hayuko pichani) akizungumzia umuhimu wa Buffer Zone kwa waendesha pikipiki hasa wanapofika katika makutano ya barabara yanayoongozwa na alama, michoro na taa za kuongozea watumiaji wa barabara. 

Meneja wa Programu wa Babarabara za TANROADS Dk.Christina Kayoza akielezea mpango mkakati wa TANROADS katika kutoa elimu ya umuhimu watumiaji wa barabara kuheshimu alama, michoro na taa za barabara ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...