Na Neema Chalila Mbuja
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula amesifu jitihada zinazofanywa na TANESCO kuhakikisha mtambo wa kuchakata gesi wa Kinyerezi unazalisha kwa ufanisi na kwa kiwango Cha Hali ya juu
Mh. Kitandula ameyasema hayo wakati kamati ya Nishati na Madini ilipotembelea kituo hicho Cha kuchakata gesi asilia na mvuke Cha Kinyerezi II ambapo pamoja na Mambo mengine ameitaka Tanesco kuendelea kuangalia vyanzo vingine vya kuzalisha umeme pasipo kutegemea maji ili kuhakikisha huduma Zinaboreka kwa wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa huduma za usambazaji umeme Mhandisi Athanasius Nangali, ameahidi kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inakuwa na tija ili kuboresha huduma.
Kituo Cha Kinyerezi kilianza ujenzi wake Machi 8, 2016 na kukamilika Machi 7 2019 ambapo ujenzi wa mradi umegharimu kiasi Cha Dola za kimarekani Milioni 344 sawa na fedha za kitanzania Bilioni648, na unazalisha Megawati 240.
Mpaka Sasa Kituo Cha kuchakata gesi Cha Kinyerezi II kina mitambo 8 inayotumia gesi asilia yaani Gas turbines ambapo Kati ya hiyo 6 unatimia gesi asilia pekee na 2 unatumia mvuke.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inatarajia pia kufanya ziara yake kwenye mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere jumamosi hii
Home
HABARI
KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA TANESCO KWA UZALISHAJI UMEME KWA KIASI KIKUBWA KITUO CHA KINYEREZI II
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...