
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) leo imeanza kampeni yake Elimu ya mlango kwa mlango katika mkoa wa Simiyu wilaya ya Bariadi yenye lengo la kuelimisha wafanyabiashara wa Bariadi juu ya masula mbalimbali ya Kodi sambamba na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu
wa wilaya ya Bariadi Bw. Lupakisyo Kapange kabla ya kuanza kwa Kampeni hiyo,
amesema amefurahishwa na ujio wa Maafisa hao kuwataka wafanyabiashara wa
wilayani hapa kuwapa mashirikiano maafisa hao watakapo watembelea maduaka yao
pia kutumia furasa hiyo kuuliza maswala na kutoa maoni yao.
“Nawashukuru
maafisa wa TRA kwa kuja kutetembelea katika kipindi hiki ambapo wilaya ya
Bariadi imekua ikipiga maendeleo makubwa na matumaini yake baada ya zoezi hili
la kungea kirafiki litawahamisiha kuendelea kulipa kodi zaidi”.
Aidha
amewasisitiza pia wafanyabiashara wa Wilaya hio inayoongoza kwa makusanyo
katika mkoa wa Simiyu kuendelea kulipa kodi kwa hiari bila ya kushurutishwa ili
kuweza kuisadia serekali kukamilisha miradi ya kuwaeletea maendeleo ya nchi
yetu sambamba na hilo amewakumbusha wafanyabiashara kuendelea kutoa risiti kila
wanapuza bidhaa au kutoa huduma na wananchi kudai risiti kila wanaponunua
bidhaa.
Aidha
kwa upande wa Afisa wa Kodi kutoka kitengo cha Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi
mkoa wa Simiyu, Bw. Benjamin Makobwe ameeleza lengo la Kampeni hiyo ni kutoa
elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na kusikiliza changamoto zao hivyo amewataka
wafanya biashara wawepe ushirikiano ili kufikia lengo la zoezi hilo.
“
leo tupo hapa mkoa wa Simiyu wilaya ya Bariadi kwa lengo la kuelimisha
wafanyabiashara wa eneo hili masuala
mbali mbali ya kodi pamoja kusikiliza changamoto na madukuduku yao kwa lengo
kuyafanyia kazi”.
Kwa
upande wao wafanyabiashara wa wilaya hio wamefurahishwa sana na kuwapngeza
maafisa wa TRA kwa kufika katika wailaya ya Bariadi kwa lengo la kuwapatia
elimu zaid katika masuali ya Kodi sambamaba na hilo walitoa wito kwa
wafanyabiashara wengine kutoa ushirikiano kwa maafisa hao na kuwaahimiza
wafanyabiashara kutoa risiti halali za EFD kila wanapouza na wananchi kudai
risiti ili kuiwezesha serekali kukusanya kodi ambayo ndio inayotumika kujenga
mashule, vituo vya afya, barabara na usamabazaji wa maji mijini na vijijini.
‘Nifurahishwa
sana na ujio wa maafisa wa TRA kwanza tumekuwa nao kama familia mja ukiwa na
familia ya upendo kama tulivyosasa sisi na TRA tutaweza kurahisisha ukusanyi wa
Kodi na kuiwezesha serikali kuleta maedndeleo zaidi”. Alisema Faida Jishiku
(mfanayabiashara).
Kampeni
ya Elimu ya mlango kwa mlango huendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) chini
ya kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
kwa kuwatembelea wafanyabiashara wa mikoa yote nchini kwa lengo
kuwapatia elimu ya kodi pamoja kusikiliza changamoto zao pamoja na maoni na
kuyafanyia kazi ili kujenga mahusiano mema na wafanyabiashara na kurahisisha
ulipaji wa kodi bila ya kukwaruzana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...