Na. OMM Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amepongeza Timu ya Wanasheria Watetezi
wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na Shirika la Maendeleo Endelevu Rukwa (
RUSUDEO) kwa kufanikisha utoaji wa Hati Za Haki Miliki za Kimila 4,530 kwa wananchi
wa vijiji vitatu vya Tambaruka, Lyele na Kisula wilaya ya Nkasi.
Pongezi hizo amezitoa leo (Oktoba 26,2022) wakati akizindua zoezi la ugawaji hati hizo
kwenye kijiji cha Tambaruka ambapo amesema zinakwenda kuwa msaada kwa
wananchi kiuchumi pamoja na kusaidia kuondosha migogoro ya ardhi.
"Naomba viongozi wa ngazi zote kuanzia wenyeviti wa vitongoji, vijiji na madiwani
shirikianeni na LEAT ili kutoa elimu kuhusu faida za hati za haki miliki za kimila ili zoezi
lisipotoshwe na watu wasiotakia mema wananchi. LEAT hawajaja kupoka ardhi yenu
bali wamekuja kupima na kuwapa hati miliki za kimila na ardhi ni umiliki wenu" alisema
Sendiga.
Kwa upande Msimamizi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili Bi. Hana
Lupembe alisema mradi huo wa miaka mitano ulianza mwaka 2020 hadi 2025
umenufaisha vijiji 18 katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga.
Mratibu huyo alitaja mafanikio mengine ni pamoja na kuwezesha halmashauri utengaji
wa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 13 kati ya 18 sawa na asilimia 86 ya
lengo na pia wametoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi 2,170 kati ya lengo
la kuwafikia watu 1,798.
Mradi huo wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili unatekelezwa na LEAT pamoja na
RUSUDEO kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani ( USAID) ambapo katika
uzinduzi wa leo umehudhuriwa na Bw. Colin Dreizin ambaye ni Mkurugenzi wa Kukuza
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga (kushoto) akikabidhi Hati ya Haki Miliki za Kimila kwa Bw. Chiluba Mwandamo mkazi wa kijiji cha Tambaruka wilaya ya Nkasi leo alipozindua zoezi la ugawaji Hati hizo jumla 4,530 zilizolewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na Shirika la Maendeleo Endeleu Rukwa (RUSUDEO) kwa ufadhili wa USAID kwenye vijiji vya Tabaruka, Lyele na Kisula.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Bw. Swagile Msananga (Kushoto) akikabidhi sehemu ya Hati za Haki Miliki za Kimila kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Queen Sendiga (kulia) leo ili azikabidhi kwa wananchi wa kijiji cha Tambaruka wilaya ya Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa zoezi la utoaji Hati ya Haki Miliki za Kimila 4,530 kwa vijiji vya Tambaruka, Lyele na Kisula wilaya ya Nkasi ziliztolewa na taasisi za LEAT na RUSUDEO .

Mkurugenzi wa Kukuza Uchumi USAID Tanzania Bw. Colin Dreizin akizungumza kwenye halfa ya ugawaji Hati za Haki Miliki za Kimila kwa wananchi wa kijiji cha Tambaruka wilaya ya Nkasi leo ambapo taasisi za LEAT na RUSUDEO zinatekeleza mradi huo kupitia ufadhili wa watu wa Marekani.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Peter Lijualikali (katikati) akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga kwa viongozi leo alipowasili kijiji cha Tambaruka kuzindua zoezi la ugawaji Hati za Haki Miliki za Kimila zilizotolewa na mashirika ya LEAT na RUSUDEO kwenye vijiji vitatu vya Nkasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...